Sehemu ya wajasiliamali wanaoishi na ulemavu wa Kusikia wanaojishughulisha na ufugaji wa nyuki na uchakataji wa asali wakiwa katika mafunzo maalum.
Meneja wa Mafunzo na Utafiti, Hamis Mwasala akitoa maelekezo katika mafunzo hayo.
Na Lydia Lugakila, Muleba
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wajasiriamali wanaoishi na ulemavu wa kusikia wanaojishughulisha na ufugaji wa nyuki pamoja na uchakataji asali wilayani Muleba na Biharamulo mkoani Kagera kumuenzi hayati Dk. John Pombe Magufuli kutokana na kuhusika pakubwa kusimamia ustawi wa wanyonge na wananchi wa chini ikiwa ni pamoja na wajasiriamali wadogo wadogo kwa lengo la kuinua uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya taifa.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mafunzo na Utafiti, Hamis Mwanasala toka shirika la viwango Tanzania -TBS katika mafunzo maalum ya watu wanaoishi na ulemavu wa kusikia kutoka wilaya ya Bihalamuro na Muleba yaliyoendeshwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Muleba- pamoja na taasisi ya maendeleo ya viziwi Tanzania (TAMAVITA) .
Mwanasala amesema mafunzo hayo kwa wajasiriamali hao ni sehemu ya kumuenzi Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwa siku zote katika uongozi wake alisimamia watu wenye maisha ya chini hasa wajasiriamali wadogo wadogo ambao wamenufaika kutokana na Serikali yao hivyo kuwataka kumuenzi kwa vitendo ili kutodidimiza uchumi wa kati hatua nzuri aliyoiacha hayati Dk. Magufuli.
Mafunzo hayo yameendeshwa na shirika la viwango Tanzania TBS ikiwa ni sehemu ya majukumu ambayo yamebainishwa kisheria kwa Sheria no 2 ya mwaka 2009 na kuwa yanashirikisha asilimia 99 ambao ni watu wanaoishi na ulemavu wa Kusikia.
Amewashauri wajasiliamali hao kuboresha biashara yao kupitia TBS ili kuifanya kuwa ya viwango.
Aidha amesema asali ni moja ya bidhaa ambayo inatumika kwa wingi ambapo hata watumiaji wengine hutumia asali Kama mbadala wa sukari ambapo wameelimishwa namna bora ya uchakataji wa asali, masuala ya afya vifungashio, usalama na unifadhi wa asali na kuwataka washiriki hao kutumia mafunzo hayo kuwa fulsa ili kunufaika ikiwa ni pamoja kuongeza thamani katika bidha hiyo huku akiahidi kuendeleza mafunzo hayo kwani sio mara ya kwanza kuletwa nchini ambapo tayari mkoa wa Mbeya, Kigoma na Tanga washanufaika na mafunzo hayo.
Aidha kwa upande wake Mgeni rasmi katika mafunzo hayo Isaya Tendega afisa biashara mkoa wa Kagera kwa niaba ya naibu waziri wa viwanda na biashara Exaud Kigahe ameipongeza TBS kwa kuratibu mafunzo hayo na kupongeza wilaya ya Muleba kwa kutoa ushirikiano kwa kundi hilo na kuwa sekta hiyo ni muhimu kwani inachangia pato la taifa kupitia shughuli za ufugaji wa nyuki na uchakataji wa asali.
"Asali yenu ikipitishwa TBS itasaidia kuwabaini wauzaji wanaochanganya vitu visivyofaa kwa mtumiaji wa asali na Kisha kufichwa baadae kumfikia mtumiaji bila kupitia TBS"alisema Tendega".
Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Henry Ruyango amelipongeza shirika hilo kwa kuleta mafunzo hayo na kuwahimiza wajasiliamali hao kuyatumia mafunzo hayo vyema ili yaweze kuwaletea fedha na kutaja uvunaji wa asali wilayani humo kuwa wa chini huku akitaja vitendo vya uchomaji moto misitu kuwa chanzo cha kupotea kwa bidhaa hiyo na kuwa nafasi pekee katika mafunzo hayo ni kufuga kisasa kuchakata asali kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na Tbs.
Hata hivyo amemuagiza Mkurugenzi wilayani humo kuhakikisha kikundi cha maendeleo ya viziwi kinasajiliwa ili kupata fedha kutoka asilimia 10 zinazotolewa kwa vikundi vingine huku akiwaomba TBS kuangalia maeneo mengine ya Mkoa huo ili kuwafikia hata ambao sio walemavu ambapo viongozi wa taasisi ya watu wenye ulemavu wa Kusikia Tanzania chini ya mtendaji wao mkuu Kelvin Nyema wameahidiwa kupewa takribani mizinga ya nyuki 200 Bihalamuro 100 Muleba 100 ambapo Kila wilaya kuanza na mizinga 50.
No comments:
Post a Comment