HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 08, 2021

UTT AMIS ILIVYOADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


Wanawake wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutoa misaada katika Mahabusu ya Watoto jijini la Dar es Salaa ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.


 Wanawake wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutoa misaada katika Mahabusu ya Watoto jijini la Dar es Salaa ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.


Meneja Mahabusu ya Watoto Upanga, Darius Damas, akizungumza na Wanawake kutoka Kampuni ya mUwekezaji UTT AMIS wakati walipotembelea Mahabusu hiyo Jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Sehemu ya vitu walivyokabidhi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake UTT AMIS, Martha Mashiku, akimkabidhi Meneja Mahabusu ya Watoto Upanga, Darius Damas, sehemu msaada wa vitu mbalimbali walivyokabidhi leo.
Kukabidhi.




Na Mwandishi Wetu

IKIWA Dunia inaadhimisha siku ya Wanawake ambapo ni kila machi 8, leo Umoja wa Wanawake wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, wametembelea Mahabusu ya Watoto Upanga na kutoa misaada mbalimbali ili kuwafariji.

Akizungumza  katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake UTT AMIS Martha Mashiku, amesema wamefika kituoni hapo kuwatazama watoto hao ikiwa ni moja ya shughuli ya kuadhimisha siku yao pamoja na kuwapatia mahitaji mbalimbali.

“Leo siku ya wanawake Duniani tumeamua kuja Mahabusu ya watoto Upanga kuangalia watoto wanaolelewa hapa wenye kesi mbalimbali ambazo zinaendelea Mahakamani. Pamoja na sisi kuja hapa tumewaletea mahitaji yao mbalimbali ambayo waliyaorodhesha kulingana na hali ilivyo kwenye kituo hiki.

“Tumeleta mahitaji kama vyakula, mipira ya kuchezea, ma feni na mahitaji mengine mbalimbali kama vyandarua kwa ajili ya kuwakinga ili wakae salama. Ili watakapo toka mahali hapa wawe watoto wema na rai wema ili kulitumikia Taifa letu huko mbeleni.” Amesema Martha.

Aidha amewataka wazazi kuhakikisha wanalea watoto katika malezi bora ili kuwaepusha ma matukio yanayoweza kuwapelekea kuvunja sheria na taratibu za nchi.

Kwa upande wake Meneja Mahabusu ya Watoto iliyopo Upanga Jijini Dar es Salaam, Darius Damas amesema wamefarijika kwa kutembelewa na akina mama hao kutoka UTT, jambo ambalo linaonyesha utu na thamani ya Mama.

“Kwa niaba ya watumishi wenzangu tumefarijika sana, UTT imejitoa, leo ni siku ya wanawake Duniani lakini wakaona waje wawaone hawa watoto licha ya kwamba watoto hawa wana kesi Mahakamani lakini wao wameona hawa ni watoto kama watoto wengine.

“Tunawashukuru sana, nitoe wito kwa jamii kwamba masuala ya malezi ya watoto ni muhimu sana, mtoto asipopata malezi stahiki, asipopata maelekezo, asipopata upendo wa wazazi anaweza mwisho wa siku akapotea.

“Niombe tukipata muda wa kuwaona watoto wetu tufanye hivyo, lakini pia tunapoondoka tuwaache katika mazingira salama hata huyo mlezi anayewaangalia awe anajua mazingira ya usalama wa mtoto”. Amesema Darius.

Hata hivyo ametoa wito kwa wazazi, walezi, jamii na taasisi mbalimbali kuwatembelea watoto ili kuwapa faraja na kutojiona kama wametengwa.

No comments:

Post a Comment

Pages