HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 08, 2021

OCODE YAWAKOMBOA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU KATIKA SHULE YA MSINGI KIBWEGERE KWA KUWAJENGEA NGAZI ZA KUPITIA

Mkuu wa shule ya msingi Kibwegere  Charles  Kulemo akiwa anazungumza na baadhi ya wazazi na walezi pamoja na walimu wa shule hiyo ambao walishiriki katika halfa hiyo.

 

 

 

NA VICTOR MASANGU, KIBAMBA

 

 

KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu na kuwathamini wanafunzi wenye mahitaji maalumu hususan walemavu Shirika  lisilokuwa la kiserikali la (OCODE ) limekuja na mpango kabambe ambapo limeweza kuwasaidia baaadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Kibwegere iliyopo kata ya Kibamba kwa kuwapatia vifaa mbali mbali pamoja na kuwajengea miundombinu rafiki ya majengo ili kuwarahisishia katika kutembea.

 

 

Akizungumza katika halfa fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kuweza kukabidhi baadhi ya miundombinu ambayo imejengwa kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalumu  Meneja wa  anayesimamia miradi ya elimu katika Manispaa ya ubungo  kutoka shirika la Ocode  Digna Mushi amebainisha kwamba utekelezaji wa mradi huo wa kutoa vifaa pamoja na kwuajengea ngazi utakuwa ni mkombozi kwa wanafunzi hao.

 

“Sisi Kama Shirika la Ocode tumekuwa tukifanya kazi ya mambo ya elimu katika manispaa hii ya Ubungo la lengo letu kubwa ni kuhakikisha watoto wetu wanaweza kusoma katika mazingira rafiki, na leo hi tupo katika shule hii ya msingi Kibwegere tumekuja kwa ajili ya kukabidhi miundombinu ya ngazi ambazo zitawez kutumika kwa wanafunzi mbali mbali amabo ni walemavu wa viungo tofauti kama vile vya mikono pamoja na miguu sambamba pia kuwapatia vifaa vitakavyoweza kuwasaidia,”alisema Digna.

 

Naye  Mkuu wa shule ya msingi Kibwegere amesema  kwamba Charles Kulemo amesema kwamba wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule hiyo wapo 15 na kwamba msaada huo wa walioupata kutoka Ocode wa kuwajengea miundombini rafiki ya ngazi itawasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kuweza kutembea kwa urahisi zaidi kwenda madarasani.

 

Mkuu huyo alibainisha kwamba shirika la Ocode limeweza kuwa mstari wa mbele katika  kusaidia kwa hali n amali katika kuboresha sekta ya elimu na kwamba msaada huo wa wa kuwajengea miundombinu ya ngazi kwa wanafunzi wa shule hiyo kutaweza kuwasaidia kwa kiais kikubwa wanafunzi ambao walikuwa wanapata shida ya kupandaili kuelekea madarasani.

 

“Katika shule yetu ya msingi ya Kibwegere kwa sasa tuna wanafunzi 15 ambao wana  mahitaji maalumu na kati yao walunana wapo tisa na wasicha wapo 6 hivyo kwa msaada huu wa shirika la Ocode la kujenga miundombinu ya ngazi ni jambo ambalo litaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wanafunzi wetu kuweza kupita kwa urahisi kwani hapo awali walikuwa wanapata shida katika suala zima la kupita.

 

Mkuu huyo katika hatua nyingine alitoa pongeza kwa Shirika la Ocode kwa kuweza kutoa msaada wa mambo mbali mbali katika shule hiyo ikiwemo kuwajengea madarasa, kuwapatia viti na meza kwa ajili ya walimu na wanafunzi lengo ikiwa ni kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri na rafiki ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingiara ambayo ni rafiki.

 

Kwa upande wake mmoja wa wakikilishi wa walezi wa watoto hao wenye mahitaji maalumu amebainisha kwamba mjukuu wake anayetambulika kwa jina la Mustafa Sefu mwenye umri wa miaka 10 alikuwa anakabiliwa na changamoto ya viungo vya mikono na miguu lakini kwa sasa anaweza kutembea kutoaka na msaada wa vifaa ambao amepatiwa.

 

Hamza Miramboi ni Mwenyekiti wa miradi wa elimu katika manispaa ya Ubungo alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha kwamba wnaunga juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu na kwamba kwa sasa wanaendelea kutoa misaada mbali mbali katika baadhi ya shule za msingi zilizopo Manispaa ya ubungo ikiwemo kuwapa wanafunzi umuhimu wa elimu jumuishi na kuwashirikika wazazi na walezi.

 

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Ocode limekuwa likiunga mkono juhudi za serikali kwa kipindi kirefu katika kuboresha sekta ya elimu hasa katika shule mbali mbali zilizopo katika Manispaa ya Ubiungo kwa kutoa vifaa mbali mbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu  ikiwemo madawati, viti, kujenga madarasa pamoja na kutoa elimu jumuishi.

No comments:

Post a Comment

Pages