Waziri wa Katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa semina ya viongozi wa dini.
Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
WAZIRI wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba amewaomba viongozi wa dini kutoa elimu kwa waumini wao juu ya kurasimisha mali zao kwa lengo la kuepuka migogoro ya kudhulumiana mali.
Pia Nchemba amesema kuwa jamii iechane na mila potofu ya kutokuandika wosia kwa kuona wanajichuria kifo na badala yake kila familia iwe na kitabu cha kumbukumbu ili kuepuka migogoro katika familia hizo pindi anapofariki baba ama mama.
Haya aliyasema jijini Dar es Salaam jana wakati akifungua semina kwa viongozi wa dini iliyoandaliwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), alisema kumekuwa na matatizo makubwa ya kudhulumiana.
Alisema semina hiyo inalenga kushauriana jinsi ya kupata maamuzi ya pamoja kuhusu umri wa ndoa pamoja na umuhimu wa kurasimisha mali ili waweza kutunga sheria nzuri zinazoendana na watanzania.
Waziri Nchemba alisema matukio yote yasajiliwe ya visazi, vifo, talaka kusajili watoto pamoja na kurasimisha shughuli ambazo baadae zinaweza kuleta mgogoro pindi mmoja wao anapofariki dunia.
"Viiongozi wa dini tusaidiane kutoa elimu kwa waumini juu ya kurasimisha mali zao kwani dunia inabadilika," alisema Waziri huyo.
Aidha Waziri huyo aliipongeza RITA kwa kutoa semina hiyo ambayo anaamini italeta mabadiliko katika jamii kupitia viongozi hao.
Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu kutoka RITA Emmy Hudson alisema kuwa lengo la semena hiyo kuwashirikisha na kuwapa elimu kuhusu huduma wanazozitoa na kuwapatia elimu pamoja na mabadiliko yanyobadilika katika huduma zao viongozi hao
"Pia tunawakumbusha viongozi wajibu wao kama viongozi wa dini katika kuteleleza majukumu yao kwa kufuata taratibu na Sheria za Usajili wa ndoa na Usajili pamoja na kupokea maoni yao ili kuboresha mahusiano yao na mawasiloano," alisema.
Kwa upande wao viongozi hao wa dini wameishukuru RITA kwa kuwapatia elimu ya namna ya kwenda kuwaelimisha waumini wao.
No comments:
Post a Comment