HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 16, 2021

Viumbe vya baharini zaidi ya 100,000 wanakufa kila mwaka kwa sababu ya uchafuzi wa Mazingira

NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


MKURUGENZI Mkuu Tume Ya Ushindani Dkt. John Mduma amesema kuwa Viumbe  vya baharini zaidi 100,000 wanakufa kila mwaka kwa sababu ya uchafuzi wa mazingira.

 

Amesema uchafuzi huo wa Mazingira unasababishwa na bidhaa za plastiki zinazotupwa baharini.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati wa kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani amesema takwimu hizo ni matokeo ya utafiti uliofanywa mwaka juzi na mtandao wa Consumers International kuhusu athari za mazingira zinaosababishwa na taka za plastiki.


Amesema hadi Kufikia mwaka 2050 kama taka za plastiki hazitadhibitiwa, idadi ya taka za plastiki baharini, itazidi idadi ya samaki, kwa sababu  zaidi ya tani milioni nane za plastiki hutupwa baharini kila mwaka. 


“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli imeanza kuchukua hatua za kupiga vita mifuko ya plastiki, ili kunusuru uhai wa viumbe vya baharini na nchi kavu,”amesema Mkurugenzi huyo.


Dkt. Mduma amesema kupitia maudhui ya maadhimisho ya siku ya haki za mlaji kwa mwaka 2021, serikali wafanyabiashara na wadhibiti ubora na usimamizi wa mazingira wanashauriwa kuchukua hatua zitakazoshaimirisha kupiga vita taka za plastiki.


Aidha amesema kwamba miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kuongeza upelekaji wa elimu kuhusu haki na wajibu wa mlaji vinavyobainisha uhitaji wa kuishi katika mazingira bora na endelevu na wajibu wa kutunza mazingira.


“Serikali ya tanzania na wizara inayosimamia uhifadhi wa mazingira inaendelea na juhudi mbalimbali za kimkakati kuhakikisha kuwa inapunguza na hatimaye kutokomeza janga la bidhaa za plastiki katika mazingira yetu,”amesema

No comments:

Post a Comment

Pages