Serikali ya India imeikabidhi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar msaada wa dawa za kutibu maradhi tofauti, ikiwemo Kensa, zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 268 za Tanziania.
Balozi
mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bhagwant Singh alimkabidhi Waziri wa
Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui
shehena ya dawa hizo katika hafla iliyofanyika Bohari Kuu ya Dawa
Marughubi.
Balozi
Bhagwant amesema mashirikiano na mahusiano ya karibu kati ya India na
Tanzania, ikiwemo Zanzibar, ulianza miaka mingi iliyopita na nchi hiyo
imekuwa ikisaidia masuala mbali mbali ya Maendeleo ikiwemo Elimu, Afya,
Kilimo na Ustawi wa Wananchi.
Ameahidi
kuwa India itaendelea kuimarisha mashirikiano yaliopo kati yake na
Tanzania kwa kutumia uwezo wa rasilimali walizonazo katika kusaidia
kuimarisha uchumi wake.
Akipokea
msaada huo, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto
Nassor Ahmed Mazrui aliishukuru Serikali ya India kwa msaada huo mkubwa
wa dawa ambao alisema utapunguza kwa asilimia tatu ya bajeti ya kuagiza
dawa nje.
Waziri Mazrui
alimueleza Balozi mdogo wa India kuwa sehemu ya dawa hizo tayari
zimepelekwa kisiwani Pemba kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa kisiwa
hicho.
Alisema Zanzibar
kupatiwa msaada huo hasa dawa za kutibu maradhi ya Kensa, ambazo ni
ghali sana kuzinunua, utasaidia sana wananchi kufuata matibabu Hospitali
za maradhi hayo Tanzania Bara na Hospitali za nje.
Alieleza
kuwa Wizara yake imeandaa utaratibu mzuri wa kielektroniki
unaohakikisha kuwa usambazaji wa dawa kutoka Bohari Kuu hadi kufika
Hospitali na vituo vya afya unakuwa na ufanisi na hazipotei njiani.
Wakati
huo huo Waziri Mazrui amemuomba Balozi mdogo wa India kuwashawishi
wawekezaji wa nchi yake kuja kuwekeza Viwanda vya Dawa Zanzibar ili
kuondosha upungufu wa dawa nchini.
Aliahidi
kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iko tayari kutoa kila aina ya
ushirikiano unaohitajika kwa muwekezaji atakaeonyesha azma ya kuwekeza
kiwanda cha dawa ili kuhakikisha lengo lake linafanikiwa.
Alisema
Zanzibar kuwa na kiwanda cha dawa ni jambo la msingi na alikumbusha
kuwa miaka ya nyuma kilikuwepo lakini kutokana na changamoto
zilizojitokeza kiwanda hicho kilisimamisha uzalishaji
No comments:
Post a Comment