HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 14, 2021

SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZASABABISHA KUTOWEKA BAADHI YA VIUMBE MUHIMU KWENYE IKOLOGIA

 

Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti, Daima Mkalimoto akifungua warsha ya mpango wa mahitaji ya usimamizi wa fedha za Bioanuai Zanzibar katika Hoteli ya Marumaru iliyopo Shangani Zanzibar.

  

Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Farhat Mbarouk akitoa ufafanuzi aiwakaribisha washiriki na wataalamu kutoka taasisi mbalimbali Zanzibar kwenye warsha ya mpango wa mahitaji ya usimamizi wa fedha za Bioanuai Zanzibar , katika Hoteli ya Marumaru iliyopo Shangani Zanzibar.


Baadhi ya washiriki wa Warsha.

 
 

Na Raya Hamad  - OMKR

Imeelezwa kuwa uwepo wa vizazi vijavyo unategemea sana ustawi wa Bioanuwai na mazingira kwani dunia imeshuhudia ongezeko la kubwa la idadi ya watu hali inayopelekea kuongezeka kwa mahitaji ya Bioanuwai za bahari na misitu

Mkurugenzi Mipango Sera na Utafiti Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi Daima Mohamed Mkalimoto ameyasema hayo kwa niaba ya Katibu  Mkuu wa Ofisiya Makamu wa Kwanza wa Rais  Bi Khadija Khamis Rajab wakati akifungua Warsha ya Mpango wa mahitaji ya usimamizi wa fedha za Bioanuai Zanzibar

Bi Khadija amesema shughuli za kibinadamu kama vile uvuli uharamu, uharibifu wa matumbawe na ukataji wa miti ovyo umechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa bioanuwai hatimae kupelekea kutoweka kwa baadhi ya viumbe muhimu kwenye mfumo wa Ikologia

Akitoa salaam kwa niaba ya mwakilishi wa  Shirika la  Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP mtaalamu  wa mradi kutoka mpango wa maendeleo wa shirika hilo Ndugu Abbas Kitogo amesema jumla ya  Nchi 36 zinashiriki katika mpango huu wenye lengo la kuwa na mfumo mzuri wa ukusanyaji wa fedha

Kitogo amewaambia washiriki wa warsha hio kuwa UNDP katika kutekeleza mpango wa mahitaji ya usimamizi wa fedha za Bioanuai imepanga kufanya shughuli nne ambazo ni kuandaa taarifa na utafiti wa kuangalia sera, taasisi katika  suala la uhifadhi wa bioanuai

Aidha kuangalia kiasi gani Serikali imewekeza katika uhifadhi wa Bioanuai,  kuangalia mahitaji na mwisho  kutengeneza mpango wa kitaifa utakoelekeza wapi waelekee katika kukusanya fedha jambo ambalo ni muhimu katika ulinzi wa Bioanuai

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira  Zanzibar Bi Farhat A. Mbarouk  amesema lengo la mpango huu ni pamoja na kuangalia changamoto za kifedha katika usimamizi na uhifadhi wa bioanuai na hatimae kuja na mfumo bora utakaosaidia uwekezaji na upelekaji wa bajeti zaidi za usimamizi wa bioanuai na mazingira kwa ujumla

Farhat amefafanua kuwa  ili kuwepo na mafanikio jambo muhimu ni kuweka utaratibu wa kuwashirikisha wadau mbali mbali na ndio maana wamewashirikisha wataalaamu kutoka taasisi tofauti ili kuona  maeneo muhimu na  kwa kiwango gani kinachotakiwa katika uhifadhi na usimamizi wa bioanui  pamoja na kuangalia mahitaji

Viongozi wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Idara ya Mazingira wameishukuru UNDP Tanzania  kwa kuichagua Zanzibar kuingia katika mpango huo wa majaribio wa kutathmini matumizi ya bajeti mbalimbali za program za maendeleo na kisekta katika usimamizi na uhifadhi wa Bioanuai

Mradi wa  Mpango wa mahitaji ya usimamizi wa fedha za Bioanuai unaotekelezwa na UNDP na kufadhiliwa na wafadhili mbali mbali ikiwemo Umoja wa Ulaya, Ujerumani, Belgium na Switzaland

No comments:

Post a Comment

Pages