Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdori Mpango, leo tarehe 10 April 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Selemani Jafo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na Mheshimiwa Hamad Hassan Chande Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, kwenye Makazi yake Jijini Dodoma
Katika mazungumzo hayo Mheshimiwa Makamu wa Rais amesisitiza juu ya utekelezaji wa haraka wa masuala ya Mungano na Mazingira likiwemo suala la Mabadiliko ya Tabia Nchi.
Makamu wa Rais Mhe, Dkt. Mpango amesema kuwa Muungano wetu ni muhimu sana hivyo ni lazima kuhakikisha kuwa Changamoto zilizobakia zinapatiwa ufumbuzi wa pamoja na kwa haraka.
Aidha Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mpango amewataka Mawaziri hao kusimamia kikamilifu suala la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa kushirikisha Wananchi na Taasisi za Serikali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. Philip Isdori Mpango, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa Selemani Jafo kushoto na Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa Hamad Hassan Chande kulia, kwenye Ofisi ya
Makamu wa Rais katika makazi yake Jijini Dodoma leo April 2021. katika mazungumzo yao Makamu wa Rais
Mheshimiwa Dkt. Mpango amesisitiza juu
ya utekelezaji wa haraka masuala ya Changamoto zilizobaki za Muungano na Mazingira
ikiwemo suala la Mabadiliko ya Tabia Nchi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
No comments:
Post a Comment