Mkurugenzi wa Taasisi ya Al-Hikma, Sheikh Nurdin Kishk
(kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe kulia wakiwakabidhi
bendera ya Taifa washiriki wa shindano la Kimataifa la Kuhifadhi Qur'an
litakalofanyika katika Uwanja wa Benyamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Al-Hikma, Sheikh Nurdin Kishk (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe kulia wakionesha mfano wa nyumba ambayo mshindi wa kwanza tapewa na Benki ya PBZ iwapo mshindi atakuwa Mtanzania katika shindano la Kimataifa la Kuhifadhi Qur'an litakalofanyika katika Uwanja wa Benyamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
NA SULEIMAN MSUYA
MSHINDI
wa Kwanza wa Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'an yanayoandaliwa
na Taasisi ya Al-Hikma anatarajiwa kupewa zawadi ya nyumba nyenye
thamani ya shilingi milioni 40.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Al-Hikma, Sheikh Nurdin Kishk
wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya
ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Sheikh Kishk amesema zawadi hiyo imetolewa na Benki ya Mwananchi Zanzibar (PBZ) iwapo mshindi wa kwanza atakuwa Mtanzania.
Amesema
iwapo mshindi wa kwanza hatakuwa Mtanzania Taasisi ya Al-Hikma itatoa
shilingi milioni 20 na zawadi zitakuwa kwa mshindi wa kwanza hadi
watano.
Kishk amesema mashindao ya mwaka huu yatashirikisha washiriki 23 kutoka nchi 21 za Bara la Afrika.
"Mashindano
ya mwaka huu yatafanyika April 25 katika Uwanja wa Banjamin Mkapa
ambapo mshindi wa kwanza akiwa Mtanzania PBZ itatoa nyumba yenye thamani
ya shilingi milioni 40.
Ila sisi kama waandaji tumetenga shilingi milioni 20 kwa mshindi wa kwanza iwapo hatakuwa Mtanzania," amesema.
Mkurugenzi
huyo ametaja baadhi ya nchi ambazo zitakuwa na washiriki ni pamoja na
Tanzania, Zanzibar, Kenya, Uganda, DRC Congo, Senegali, Afrika Kusini na
Burundi.
Aidha amesema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar, Dk.A
Hussein Mwinyi na Mgeni Maalum atakuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Sheikh
Kishk amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye mashindao hayo
ambayo yamekuwa na mafanikio makubwa kwa miaka 20 iliyopita.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe ameipongeza Taasisi
ya Al-Hikma kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yanachangia kujenga
jamii yenye kumcha Mungu na nidhamu.
Gondwe amesema wilaya itatoa ushirikiano wa hali ya juu kuhakikisha mashindani hayo yanafanyika kwa usalama na mafanikio.
"Nawapongeza
Al-Hikma kwa kuandaa mashindao haya kwani yamekuwa na matokeo chanya
tangu yaanze. Naomba washiriki wa Tanzania mjitahidi kubakiza ushindi
hapa," amesema.
Aidha,
Mkuu wa Wilaya Gondwe amewataka wafanyabiashara kuacha tabia ya kuongeza
bei ya bidhaa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment