Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza jambo na baadhi ya viongozi mbali mbali katika kikao maalumu cha kufanya tathimini ya tatu mkataba wa mambo yanayohusiana na lishe ngazi ya Mkoa ambapo kimewajumjuisha viongozi mbali mbali wa ngazi za Wilaya na Mkoa. (PICHA NA VICTOR MASANGU).
VICTOR MASANGU, PWANI
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo amewaagiza wakuu wote wa Wilaya zipatazo saba kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kuweka mipango madhubui ya kusimamia ipasavyo changamoto zilizopo katika baadhi ya maeneo kwa kuwepo kwa lishe duni kwa wananchi na udumavu, hali ambayo amesema inaweza kupelekea kukwamisha shughuli za kila siku katika kuleta mambo ya kimaendeleo hivyo ametaka hali hiyo ikomeshwe.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao maalumu cha kufanya tathimini ya tatu mkataba wa mambo yanayohusiana na lishe ngazi ya Mkoa ambapo kimehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali, wadau wa maendeleo, waganga wakuu wa Wilaya, wenyeviti wa halmashauri zote tisa, wakuu wa Wilaya sambamba na wakurugenzi.
Ndikilo alisema kwamba huduma ya masuala ya lishe yanapaswa kutiliwa mkazo wa wa hali ya juu hivyo wakuu wote wa Wilaya za mkoani Pwani wanatakiwa kutekeleza mkataba huo kwani kuwepo kwa lishe bora ni kichocheo kikubwa katika maendeleo endelevu katika nyaja zote hasa katika sekta ya viwanda pamoja na kilimo.
“Ndugu zangu suala la lishe katika Mkoa wa Pwani ni muhimu sana kwa sababu usipokuwa na afya njema uwezi kufanya kazi yoote ile wakati mwili wako ukiwa legelege na kwamba hata katika sekta ya kilimo uwezi kulima ukiwa haupo vizuri, hivyonawaagiza wakuu wangu wa Wilaya jambo hili mkalisimamie ipasavyo na kuna baadhi ya wilaya katika jambo ili hamjafanya vizuri kabisa,”alisema Ndikilo.
Pia Ndikilo ametumia fursa ya kikao hicho kuwahimiza wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Pwani kuachana na tabia ya kupandisha bei kiholela hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kwaamaba wahakikishe wanazingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa katika suala zima la uuzaji wa bidhaa zao na kwamba wananchi wazidi kumwombea Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika kuwaongoza vema wananchi wa Tanzania ili kupata baaraka kubwa.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere amewahimza viongozi mbali mbali wa Wilaya ambazo hazijafanya vizuri kujitahidi zaidi katika mambo mb ali mbali yanayohusiana na lishe hasa kwa wananchi wote wa waeneo yao ili kuondokana na changamoto hizo ambayo ipo katika baadhi ya Wilaya.
“Kwa kweli suala la mambo ya lishe katika Mkoa wetu wa Pwani ni jambo amablo lipo nyeti sana kwa hivyo ninawaomba viongozi wote katika ili tuweze kushirikiana kwa pamoja kwa lengo wa kuwahimiza wananchi juu ya umuhimu mkubwa katika mambo mbali mbali ya mambo ya lishe na manufaa yake ,”alisema Dk, Mgere.
Dk. Magrere alifafanua kuwa ana imani kubwa endapo viongozi wa Wilaya kwa kushirikiana na wananchi wao wanaweza kuweka mipango madhubuti pamoja na kuwa bega kwa bega na watalaamu mbali mbali ambayo yataweza kusaidia kuleta mabadiliko katika Nyanja mbali mbali hasa katika mambo ya lishe.
“Napenda kuchukua fursa hii ya kuwakumbusha viongozi wa baadhi ya Wilaya ambazo kwa namna moja hama nyingine sehemu zao ambazo wanazifanyia kazi hazijafanya vizuri sana katika suala la lishe ambalo leo tumeakua kukutana kwa pamoja na viongozi wa halmashauri zote tisa za Mkoa ili kuweza kuona namna ya kulijadili na kulitafutia ufumbuzi,”aliongeza Dk. Magere.
Nao baaadhi ya viongozi na wadau ambao wameshiriki katika kikao hicho wameahidi kuyafanyiakazi maagizo yote ambayo yametolewa na kwamba wataweka mipango madhubuti ambayo katika siku za usoni itaweza kubadilisha kabisa chanagmoto ambazo zinawakabili katika mambo ya masuala ya lishe ili wananchi wasiwe wadumavu.
Kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kuweza kujadili mikakati ya kusaidia mambo mbali mbali yanayohusiana na lishe ikiwemo kujadili changamoto zilizopo katika halmashauri zote tisa za Mkoa wa Pwani ili kuweza kuzitafutua ufumbuzi wa kudumu.
No comments:
Post a Comment