HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 18, 2021

Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ifanyiwe marekebisho ili kuwakomboa watoto wa kike

NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


MAREKEBISHO  ya haraka yatakiwa kufanyika katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971 hususani vifungu  vya  13 na 17 kwani vimepitwa  na wakati  na inatoa idhini ya watoto wa kike kuolewa wakiwa chini ya umri wa miaka 18.

Akizungumza leo Jumamosi  April 17 wakati wa majadiliano yaliyoandaliwa na Taasisi ya Msichana Initiative  juu ya vifungu vya 13 na 17 vya sheria ya ndoa, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba    Sheria Najma Giga amesema  umefika muda Muafaka wa Bunge  kufanya marekebisho ya sheria hiyo kwani imekuwa na mapungufu makubwa hivyo watajitahidi iweze kufanyiwa marekebisho hususani kifungu cha 13 na 17.


“Sasa umefika muda muafaka sheria hii kuangaliwa na sisi Wabunge tunatakiwa kupaza sauti na kuifanyia marekebisho sheria hii kwani watoto wetu wa wanaolewa katika umri wa chini ya miaka 18 na mfano ni kwangu mwenyewe mama yangu aliolewa akiwa na umri wa miaka 14,”amesema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Manyoni Magharibi,Elibariki Kingu (CCM) amesema kifungu hicho kimekuwa kichaka cha baadhi ya watu kuficha mambo yao kwani kuna baadhi ya mabinti wamekuwa wakipewa mimba na kisha wahusika kuwaoa ili kuficha makosa yao.

Amesema Tunataka sheria isimame kwa wote kutambua katika suala zima la kumlinda mtoto wa Kike a wakiume kwa pamoja.

" Unakuta mtoto anapewa mimba akiwa chini ya umri wa miaka 18 ili kupunguza makali ya kesi utakuta  mhusika anamuoa kwa kisingizio cha sheria hiyo,”amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Msichana Initiative,Rebeca Gyumi amesema  mara baada ya wao kupaza sauti sasa ni zamu ya Wabunge kuhakikisha vifungu hivyo vinafanyiwa marekebisho ili umri wa mtoto wa kike kuolewa uwe kuanzia miaka 18.  

“Kamati hii ni muhimu kama wadau tumekuja kuongea nao ili tuweze kurekebisha kipengele cha 13 na 17 kinachoruhusu mtoto  wa kike kuolewa kuanzia miaka 18 na kuweka umri wa usawa kwa mtoto  wa umri wa miaka 18, tunaamini kutokana na mazungumzo yetu kamati imetusikiliza tunasema siku zote ni zamu ya wabunge kwahiyo tupo tayari kutoa sauti,”alisema.

Naye,Mbunge wa Viti Maalum,ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria Asha Abdalla Juma ‘Mshua’ (CCM)  alisema umefika muda muafaka wa kupiga vita mila potofu na kumsaidia mtoto wa kike kuingia katika ndoa akiwa anajitambua.

No comments:

Post a Comment

Pages