Makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa pia na Katibu wa ACT Wazalendo wa Mkoa wa Kichama wa Selou Ndugu Mtutura Abdallah Mtutura ni utekelezaji wa ahadi yake kwa viongozi hao aliposwali Sala ya Idd El Fitr Msikitini hapo.
Ado Shaibu aliwapongeza viongozi na waumini kwa jitihada wanazozifanya kujenga msikiti mpya utaoendana na mahitaji ya sasa Kijijini hapo. Aliwaahidi kuwa yeye Mwenyewe na kwa kushirikiana na marafiki atawasaidia kuhakikisha kuwa msikiti huo unakamilishwa.
Akiwasilisha Saruji hiyo, Ndugu Ado amesema kuwa atawashirikisha marafiki zake zaidi ili kuhakikisha mahitaji mengine kama vile kokoto, nondo, mbao, bati n.k yanapatiwa ufumbuzi ili Waislamu wa Msinji waweze kuswali kwenye msikiti bora.
No comments:
Post a Comment