Meneja Mwandamizi wa Bima Benki ya NMB, Catherine Joshua akibofya kitufe
kumpigia mmoja wa washindi kwenye shindano la 'Bonge la Mpango' droo ya
saba iliyofanyika leo Tawi la NMB Mbezi Louis jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Ofisa Mkaguzi toka Bodi ya Michezo
ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga na Afisa Huduma kwa
wateja Benki ya NMB, Neema Kazaviyo (kulia) wakishuhudia.
Meneja Mwandamizi wa Bima Benki ya NMB, Catherine Joshua akizungumza
kwenye shindano la 'Bonge la Mpango' droo ya saba iliyofanyika leo Tawi
la NMB Mbezi Louis jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkaguzi toka
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT),
Elibariki Sengasenga na Afisa Huduma kwa wateja Benki ya NMB, Neema
Kazaviyo (kulia) wakishuhudia.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mbezi Louis, Nestory Mwombeki (kushoto)
akizungumza kwenye shindano la 'Bonge la Mpango' droo ya saba
iliyofanyika leo tawini hapo. Wa pili kushoto ni Ofisa Mkaguzi toka Bodi
ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki
Sengasenga, Meneja Mwandamizi wa Bima Benki ya NMB, Catherine Joshua na
Afisa Huduma kwa wateja Benki ya NMB, Neema Kazaviyo wakiwa kwenye
hafla hiyo.
NA MWANDISHI WETU
WASHINDI
12 wa droo ya saba ya Kampeni ya Weka Akiba na Ushinde 'NMB Bonge la
Mpango', inayoendeshwa na Benki ya NMB, wamepatikana leo, wakiwemo
wawili waliojinyakulia pikipiki za miguu mitatu aina ya Lifan Cargo.
Droo
hiyo imefanyika kwenye Tawi la Mbezi Louis jijini Dar es Salaam, ambako
idadi hiyo inafanya jumla ya wateja 82 kunufaika na NMB Bonge la
Mpango, wakiwemo 70 waliojinyakukia pesa taslimu (hadi wiki saba) na
washindi 14 waliotwaa zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu.
Akizungumza
kabla ya kufanyika kwa droo hiyo, Meneja Mwandamizi wa Bima wa Benki ya
NMB, Catherine Joshua, amesema hadi sasa wametoa zawadi zenye thamani
ya zaidi ya Sh. Mil. 109, tangu kuanzishwa kwa NMB Bonge la Mpango -
kampeni itakayotoa zawadi za Sh. Mil. 550 hadi itakapofikia ukomo.
"NMB
Bonge la Mpango ni kampeni inayo hamasisha utamaduni chanya wa uwekaji
akiba, ambako washindi 10 kila wiki hujishindia pesa taslimu, pamoja na
pikipiki ya Lifan Cargo (mbili kila wiki), sambamba na gari dogo ya
mizigo (maarufu Kama Kirikuu) katika droo za kila mwezi.
"Pia,
imo zawadi kuu ambayo ni ya gari la kifahari aina ya Toyota Fortuner
yenye thamani ya Sh. Mil. 169. Wito wetu kwa wateja wetu ni kuendelea
kuweka akiba inayoanzia Sh. 100,000 katika akaunti zao na kwa wasio na
akaunti, kufungua na kuweka akiba kuanzia kiasi hicho ili kujiwekea
nafasi ya kushinda," alisema Catherine.
Kwa
upande wake, Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania
(GBT), Elibariki Sengasenga, aliwahakikishia wateja wa NMB kuwa Bonge la
Mpango ni kampeni inayoendeshwa kwa mujibu wa sheria, ikizingatia
taratibu zote na kuwataka kushiriki bila hofu, kwani inafanyika chini ya
usimamizi wao.
"Niko
hapa kwa ajili ya kusimamia droo hii, ambako ni jukumu letu kama Bodi
yenye dhamana. Niwahakikishie washiriki kuwa kampeni hii inatoa washindi
kwa kufuata taratibu zote, wito wetu kwao ni kuendelea kujiwekea akiba -
ambacho ni kigezo kikuu cha kupata nafasi ya kushiriki," alisema
Sengasenga.
Katika droo hiyo, waliojinyakukia pesa taslimu (kiasi walichoshinda na matawi yao kwenye mabano) ni: Imelda Christopher Laizer na Annastazia George Lukinga (500,000), Marietta Kashindye Ndanshau (129,391.60), Mary Tungucha (300,000), Sawiya Rashid Mtawala ( 407,200 ).
Washindi wengine wa pesa taslimu wa droo ya saba ni: Joyce Massawe Edesi (298,200), Linus William Rwinwa (298,200) Jonas John Dasare (202,300) ,Bernadetha Philipo William (304,200) na Letinga Matangi Lyama ( 104,933)
Katika
droo hiyo, washindi wawili walioshinda pikipiki za Lifan Cargo walikuwa
ni EMMANUEL ENOS MWAVIPA Mkazi wa BARIADI na KIJIWE MISHKAKI.
NMB
Bonge la Mpango ni kampeni ya miezi mitatu iliyozinduliwa mapema mwezi
wa tatu (Machi) mwaka huu, ambako licha ya kuhamasisha utamaduni chanya
wa kuweka akiba, inatumiwa pia na Benki ya NMB kurejesha kwa jamii
sehemu ya faida yake ya mwaka.
No comments:
Post a Comment