Kapteni Selemani Semunyu (kushoto) akichukua futari akifuatiwa na katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Hassan Abbas na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam wakati wa Ftari ya Mabondia Jana Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Mchezo wa Ngumi waliohudhuria Ftari ya Mabondia iliyoandaliwa na kapteni Selemani Semunyu kwa ajili ya mabondia wakifuatilia matukio katika ukumbi wa JWTZ 361 Mwenge Jana Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Hassan Abbas (katikati) akizungumza na Kapteni Selemani Semunyu ( Wakwanza kulia) na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Musa ( wakwanza kushoto) juu katiaki ni Bondia Dulla Mbabe wakati wa Ftari ya Mabondia Jana Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Hassan Abbas (katikati) akiwa katika Picha ya pamoja na Baadhi ya wadau wa Mchezo wa Ngumi waliohudhuria Ftari ya Mabondia iliyoandaliwa na kapteni Selemani Semunyu Jana Jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imeahidi kutoa ushirikia kufanikisha Pambano la Masumbwi kati ya Mabondia Mahiri Nchini Twaha Kiduku na Dulla Mbabe litakalofanyika Julai 24, 2021 Jijini Dar es Salaam.
Hayo
yalisemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Dk Hassan Abbas wakati wa Futari kwa Mabondia iliyoandaliwa na Wakala
wa Michezo wa PeakTime jijini Lugalo Jijini Dar es Salaam.
"
hili tunalibeba hakuna kusubiri na natoa wito kwa wadhamini kujitokea
kutumia nafasi hii kujitangaza kwa kuleta maslahi kwa washiri. Alisema
Dk. Abbas.
Aliongeza
kuwa mbali na kutoa ushirikiano pia aliahidi kufikisha ombi kwa Waziri
Mkuu Mh Kassim Majaliwa kuwa mgeni rasmi katika pambano hilo.
Kwa
upande Mwingine alisema wameanza kutenga fedha kidogo kidogo ili
kusaidi wanamichezo wanaosafiri nje ya nchi kuwakilisha Taifa.
Upande
wake Mwakilishi wa Peaktime walioandaa Futari hiyo Kapteni Selemani
Semunyu alisema maandalizi kuelekea Pambano hilo yako sawa na uwepo wa
Waziri mkuu utaupa hadhi mchezo na kufungua fursa nyingi kwa wachezaji
ambao wengi hutoka familia duni.
Tunaendelea
kutafuta Wadhamini ili ikifanikiwa Waziri Mkuu aje kukabidhi gari
zawadi ambayo tunaamini itakuwa chachu katika Mchezo huo na tunaamini
wadhamini watajitokeza. Alisema Kapten Semunyu.
Kwa Upande wake Mwakilishi wa
Kamisheni
ya Kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania TPBRC Yahaya Poli ameipongeza
Peaktime na kuwaomba wadau wengine kuiga mfano huo kwani unaipa heshima
tasnia.
Kwa
upande wake Mwakilisho wa Mabondia Hussuen Itaba alisema hatua kubwa
sasa imefikiwa katika mchezo wa Ngumi na Kuitaka peaktime kuendeleza
ilikofikia.
Mmoja
wa Wadhamini wa Iftari hiyo Peter Kinabo kutoka Euromax alisema
Majukumu ya Kijamii ni matukio muhimu yanayotakiwa kuendelezwa nao
Eoroma wameamua kusaidia katika Ngumi.
No comments:
Post a Comment