NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
KATIKA
kuwepo kwa malalamiko ya wananchi kuhusu kupanda kwa gharama za
vifurushi Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeishauri
Serikali kuona haja ya kuangalia upya suala la huduma za vifurushi.
Hayo
yamesemwa leo jijini hapa na katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM) Raymond Mwangwala wakati akizungumza na waandishi wa
habari baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza kuu la umoja wa vijana
CCM.
aidha
ameishauri Serikali kuona haja ya kuangalia upya suala la huduma za
vifurushi kwa kulichukulia kwa umakini ili kuokoa ajira kwa vijana
waliojiajiri katika uchumi wa kidigitali.
"sisi
kama vijana wa CCM tunaishauri serikali ,vijana wetu wanaelekea
kukosa ajira kutokana na gharama kubwa za bando,tunaiomba Serikali yetu
tukufu kuona namna ya kuboresha changamoto ya huduma za vifurushi
kupitia mitandao ya simu;
Kwani
uwepo wa gharama za juu katika manunuzi hukwamisha vijana kukua
kiuchumi kutokana na wengi kufanya shughuli zao kupitia mitandao ya
kijamii,"amesema
pia
baraza kuu limemvua uongozi Hussen Salehe aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM
wa wilaya ya moshi vijijini kwa kutokuwa na maadili pamoja na nidhamu
baada ya kupokea mapendekezo yaliyowasilishwa katika kikao cha
halmashauri kuu ya ccm ya mkoa wa Kilimanjaro.
"Baraza
kuu lilijiridhisha,Kamati ilijiridhisha na kuona kwamba kwa tuhuma zile
na mapendekezo yaliyotolewa katika kikao halmashauri kuu ya mkoa hivo
limemvua uongozi,
“Hivyo naagiza mkoa wa Kilimanjaro kutangaza nafasi ya mwenyeki wa uvccm, katika wilaya ya moshi vijijini”amesema.
Sambamba
na hayo UVCCM pia imeazimia kumuenzi hayati Dkt. John Magufuli
aliyekuwa Rais wa awamu ya tano kwa kuyaendeleza yale yote mazuri
aliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wake.
Lakini
pia wamempongeza Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kwa kuweza
kuteuliwa kwa ushindi mnono huku akiwawataka vijana kuunga mkono
jitihada zinazofanywa na Rais Samia pamoja na serikali yake.
Tutamlinda
,tutamtetea Rais wa chama chetu iwe mvua au jua,pia kwa kuongeza juhudi
katika kufanya kazi na uzalendo katika nchi yetu
Pia
wamempongeza Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wote walio chaguliwa
kuunda sekretarieti mpya ya chama chetu,tunaimani kubwa nao,tupo tayari
kushirikiana nao kwa maslahi ya chama chetu kwa kazi nzuri pia
tunakiopongeza chama chetu kwa kazi nzuri ya kusimamia cham,a chetu.
No comments:
Post a Comment