NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
MWENYEKITI
wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM),Kheri
James ameiomba serikali kuitafutia ufumbuzi kero ya kupanda kwa gharama
za virushi vya Internet (bando), ili kuokoa ajira za vijana wengi
waliojiajiri.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati alipokuwa akifungua kikao cha Baraza kuu la umoja wa Vijana .
Amesema
kuwa, kupanda kwa gharama za vifurushi nchini kuna mchango mkubwa kwa
vijana wengi kupoteza ajira zao ambao walikuwa wamejiajiri kupitia
mifumo mbambali ya Internet.
“Sio
kila anayetumia Internet ni kwa ajili ya kuperuzi tuu meseji mitandaoni
wengi hivi sasa wanatumia Internet kwa ajili ya kutangaza biashra zao,
kusoma na mtandao hivi sasa ni biashara hili suala lisifumbiwe macho
serikali lazima iongeze juhudi katika kutafuta ufumbuzi na kuja na njia
itakayo leta nafuu kwa watumiaji”amesema James
Kadhalika
amesema kuwa kuna vijana wengi ambao wamejiajiri kupitia mitandao ya
kijamii ambao walikosa ajira serikalini, hivyo ipo haja suala hilo
kutafutiwa ufumbuzi wa haraka na kuleta nafuu kwa watumiaji.
“Jambo
hili serikali tunaona inalifanyia kazi lakini tunaomba juhudi iongezwe
kwani vijana wengi wamejiari na wengine kuajiliwa kupitia mitandao ya
kijamii, kuna watu wanatangaza bidhaa zao lakini bando ni kikwazo.
“Hatuwezi
kuzungumzia Tehama kama hakuna mtandao, hatuwezi kuzungumzia teknolojia
kama hakuna matandao wala hatuwezi kuzungumzi mambo ya ubunifu kama
bando itakuwa ni kikwazo hivyo tunaomba serikali itafute suluhu ya
uhakika kuhusu jambo hili”amesisitiza James
Mwenyekiti
huyo pia aliomba serikali kuhakikisha inaondoa urasimu na ukilitimba
katika masuala ya uwekezaji kwakuwa hawanga wakubwa katika kero hiyo hua
ni kundi la vijana.
“Katika
suala la uwekezaji hapa kama serikali itaweka ukilitimba basi wahanga
wakuu watakuwa ni vijana na sisi hatupendi hili litoke hivyo basi ni
vizuri kila halmashauri kuwa na mikakati yake ya uwekezaji kwa
kuwatafuta wawekezeji na siyo kuendelea kusubiri waje”amesema
Pia,
aliitaka serikali pamoja na kutoa kipaumbele kwa wawekezaji kuhakikisha
kuwa ajira za wazawa zinalindwa kwa gharama yoyote ile.
“Hatutaki
kuona katika uwekezaji vijana wetu wanakuwa manamba kwa kupatiwa ajira
za ulinzi na ufagiaji tuu bali tunataka kuona vijana wetu wanakuwa na
nafasi kubwa katika makampuni hayo”amesema
Vile
vile, amesema kuwa Baraza kuu hilo linamapongeza Rais Samia Suluhu
Hassan, kwa kuchaguliwa kwa asilimia 100, kuwa mwenyekiti wa chama cha
Mapinduzi (CCM) Taifa.
Amesema UVCCM, itampaushirikiano wa kutosha katika kipindi chote ili kuendelea kuitekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Katibu
Mkuu wa Jumuiya hiyo Taifa, Raymond Magwala, amesema kikao hicho
kitakuwa na mambo makuu mawili moja ikiwa ni uchaguzi kwa ajili ya
kujaza nafasi za wajumbe wa halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi (NEC)
bara na visiwani.
No comments:
Post a Comment