Mwenyekiti wa kamati ya elimu afya na maji na diwani wa kata ya Rulanda Evart Ernest Tilwetwa.
Na Lydia Lugakila, Muleba
Madiwani
katika Halmashauri ya Muleba mkoani Kagera wameendelea na taarifa
rasmi za kuwatafuta wahusika waliowabebesha mimba wanafunzi wa shule za
msingi na sekondari wilayani humo huku watu 16 wakiwa wanasakwa na
mmoja kukamatwa kwa matukio hayo.
Ikiwa jumla ya kesi 32
zimeripotiwa na mtu mmoja kutoroka, tayari kesi 3 ziko mahakamani na
kesi moja imehukumiwa ambapo shule wanazotoka wanafunzi hao
waliobebeshwa mimba ni jumla ya shule 23 zikiwemo msingi na sekondari.
Akieleza
taarifa hiyo katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya
wilaya ya muleba Evart Ernest Tilwetwa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya
elimu afya na maji pia diwani wa kata ya Rulanda amesema kuwa kutokana
na uwepo wa wimbi la wanafunzi kubeba mimba kwa shule za msingi na
sekondari katika baadhi ya wilaya mbalimbali mkoani Kagera wilaya hiyo
iliunda kamati maalum ambayo kazi yake kubwa ni kuhakikisha inafuatilia
kuzuia na kudhibiti mimba shuleni, ikiwa ni pamoja na watu wanaohusika
kubebesha mimba wanafunzi walifuatiliwa na kukamatwa na baadhi yao
kupelekwa katika vyombo kisheria.
Amesema kuwa kamati hiyo ilifanikiwa kukamatwa kwa mtu mmoja na mmoja kutoroka huku 16 wakiendelea kusakwa.
Evert
ameongeza kuwa, kufuatia mikakati kabambe waliyonayo madiwani hao kwa
kushirikiana na wadau pamoja wananchi wameendelea kuhamasisha na
kuonyesha madhara ya mimba idadi ya wanaobeba mimba mwaka baada ya
mwaka imeendelea kupungua toka mwaka 2019 hadi Aprili 2021.
"
shule za msingi kwa mwaka 2019 walibeba mimba wanafunzi 7, sekondari
wanafunzi 22 jumla 29 ambapo mwaka 2020 shule za msingi walipungua hadi
kufikia 5 sekondari 18 jumla yake 23 na hadi mwaka 2021 mwenzi aprili
shule za msingi hakuwepo mwanafunzi hata mmoja aliyebeba mimba huku
sekondari wakiwa 5" alisema diwani huyo.
Aidha amesema kuwa
jitihada hizo zimeleta ufanisi mkubwa katika wilaya hiyo licha ya ugumu
huku akitaja changamoto kubwa inayosababisha kufifisha jitihada hizo
kuwa ni pamoja na wazazi wa mabinti kwani pale inapotokea mtoto kabeba
mimba na wakaonekana ofisini viongozi uchukua hatua za kuwapeleka katika
vyombo vya sheria, ambapo baadae wahusika waliombebeshwa mimba
mwanafunzi upita mlango wa nyuma na kukutana na wazazi wa familia ya
mwanafunzi ili wakatoe chochote na kesi ipuuzwe au wakati mwingine binti
anakuwa hajulikani halipo na yule aliyembebesha mimba hapatikani jambo
linalosababisha ushirikiano kukosa.
Hata hivyo diwani Ernest
amesema madiwani hao wataendelea kutoa elimu katika jamii ikiwa ni
pamoja na kuchukua hatua za kuwabaini na kuwakamata na kuwafikisha
katika vyombo vya sheria wote wanaohusika na matukio hayo na kuongeza
kuwa tayari wamebaini kundi la waendesha pikipiki maarufu BODA BODA na
vijana wa kawaida wenye uwezo na wamiliki wa vioski wanafanya ushawishi
kubwa kwa watoto hao.
No comments:
Post a Comment