HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 31, 2021

WAZALISHAJI WA MAZIWA TANGA WAJIUNGA NA NHIF KWA KUWEZESHWA NA BENKI YA CRDB

Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kushoto akiwa Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF, Christopher Mapunda kulia wakisaini  makubaliano na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF  wataweza kunufaika na mpango wa Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union(TDCU) kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa halfa ilifanyika Jijini Tanga.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kulia wakibadilishana hati za makubaliano na Mwenyekiti wa  TDCU Shamte Saudi mara baada ya kuingia makubaliano hayo wanaoshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Jackline Senzighe.

 

WAZALISHAJI wa Maziwa Tanga mjini wataanza kunufaika na mpango wa Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union(TDCU).

Hatua hiyo inatokana na kuingia makubaliano na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF waliingia siku chache zilizopita za kuwawezesha wana ushirika kujiunga na bima ya afya kwa utaratibu wa Ushirika Afya. 

Katika makubaliano hayo, Benki ya CRDB itamlipia mwana ushirika michango ya bima ya afya kwa wakati na mwana ushirika huyu atairejesha bila riba wakati wa msimu wa mauzo. 

Akizungumza katika uzinduzi wa mpango huo, Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda amesema kuwa ushirikiano huo na Benki ya CRDB ulianza tangu Mei 5, 2021 kwa pande zote mbili kusaini Makubaliano ambayo yatawawezesha wanachama walio kwenye Vyama vya Ushirika kunufaika na huduma za matibabu kupitia bima ya afya bila kuwa na changamoto ya kifedha.

 

“Mfuko umeazimia kuwafikia watanzania wote na huduma za Bima ya afya ili waweze kupata huduma za matibabu kwa urahisi ndio maana tumekubaliana na Benki ya CRDB ambao ni wadau wakubwa wa wana ushirika nchini kuwawezesha wana ushirika kujiunga na bima ya afya bila changamoto ya kifedha”alisema Mapunda.

 

Akizungumzia huduma, Mapunda alisema kuwa mwana ushirika na familia yake atapata huduma zote za matibabu katika mtandao mpana wa vituo zaidi ya 8,000 Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitali ya Taifa.

 

Akizingumza katika tukio hilo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts amesema Benki ya CRDB iko mstari wa mbele katika kuhudumia wana ushirika kwa namna mbalimbali na sasa inamwezesha mwana ushirika kujiunga na bima ya afya kwa kulipia michango yake kwa mwaka ili wakati wa mauzo ndipo airejeshe bila riba yoyote juu yake.

 

“Tunaungana na Serikali yetu katika kuhakikisha wana ushirika nchini wanafanikiwa kwa kuwa na uhakika wa matibabu na katika hili Benki ya CRDB tutamchangia mwana ushirika mchango wa bima ya afya wa mwaka wa Shilingi 76,800 na mwenza wake kiwango hicho hicho na kwa kila mtoto Shilingi 50,400 kwa mwaka.

 

Alisema nia yao ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Watanzania wote wanakuwa na bima ya afya kama ambavyo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza na tumeanza na kundi la wana ushirika kwa sababu ndio sekta inayoajiri watu wengi zaidi nchini” alisema Dkt. Witts.

 

Akizungumzia huduma za Benki ya CRDB alisema Wana ushirika hawata pata shida ya huduma za kibenki kwa kuwa ina mtandao mpana wa matawi 246, wakala zaidi ya 19,000 na ATM 550 nchi nzima hivyo ni rahisi kwao na wananchi wengine kupata huduma kwa karibu zaidi.

 

Mpango huu unazinduliwa kwa Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini ukiwa ni mwendelezo wa kuwafikia wana ushirika wote nchini hivyo wanachama kupitia Vyama vyao vya Ushirika wanahimizwa kujiunga kwa kuwa ni wa manufaa, hauna riba yeyote kwa mkulima na wanarejesha michango ya bima ya afya baada ya mauzo ya bidhaa husika.

 

Tangu kuanza kwa ushirikiano huu baina ya NHIF na Benki ya CRDB Mei 5, 2021, vyama vya Chunya Tobacco-growers Cooperative Union (CHUTCU), Maziwa Cooperative Union (MCU), Muungano wa Wauza Maziwa wa Rungwe (MWAMARU) na Tanga Diary Cooperative Union (TDCU) vimeshaanza kunufaika na tunategemea vyama vingi zaidi kujiunga na kunufaika na mpango huu.

 

Awali akizungumza wakati tukio la kutiliana saina kwa ajili ya kutekeleza makubaliano Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alisema hilo ni jambo nzuri na lenye tija kubwa kwa kwa manufaa zaidi ya wazalishaji wa maziwa mkoani humo

 

DC Mwilapwa Benki ya CRDB na NHIF kwa jinsi walivyokuja na mpamgo huo utasaidia kuleta  manufaa makubwa kwa wananchi kutokana na kwamba dira ya Taifa ya maendeleo 2020/2025 inaeleza kwamba itakapofika 2025 watanzania wote wawe wameingia kwenye mpango utakaowahakikishia wanaweza kupata huduma ya afya wakati wowote bila kujali vipato vyao.

 

“Wakati huo utakapofika kwenye lengo hilo namna peke yake kuhakikisha watanzania wanapata tiba bila kupitia vipato vyao ni kupitia huduma ya afya hivyo ni wazo jema kutekeleza azma ya serikali lakini kutekeleza mambo makubwa lazima uwe na uwez,i rasiliamali fedha”Alisema

 

Mkuu huyo wa wilaya aliwapongeza kwa mpango huo ambao alisema unaitoa kimasomaso Serikali watanzania ni jambo jema watokee watu ambao wanakubaliana nalo nao ni Benki ya CRDB ambao wamesaidia kuwezesha kwenye uwezeshaji wa kifedha.

 

 “Mmewezsha mkopo usio na riba mnapofanya hilo hamtekelezi lile la 2020/2025 ambalo ni la Tanzania lakini mnatekeleza malengo ya maendeleo endelevu ambavyo yanafikia mwaka 2030 wenzetu umoja wa mataifa wanafikiria dunia watu wote wawe wameingia kwenye mpango wa bima ya afya lakini sisi tunasema kabla ya wengine wote duniani hawajafikia tutakuwa tumefika 2025”Alisema DC Mwilapwa.

 

Alisisitiza kwamba Mfuko wa Bima ya Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wamefanya kazi yao kutekeleza agizo la serikali na CRDB wanafanya kazi kusaidia jitihada za mfuko huo lakini jambo jingine mliloliangalia ili unufaike lazima uwe mwana ushiriki hivyo watakwenda kuona maendeleo makubwa kwenye ushiriki kwa kupatiwa bima ya afya,

 

Naye kwa upande wake Mrajis wa vyama vya Ushiriki mkoa wa Tanga Jacquiline Senzighe  alitoa shukruani kwa mwelekeo uliopo mbele yao wa kuwa na bima ya afya kwa wafugaji lakini mpango huo unategemewa kwenye ushiriki wote na hizo ni habari njema zenye manufaa makubwa kwao.

 

Alisema kwa sababu wanaushirika lazima watoke ili waweze kutoka wanapaswa kuwa na afya njema huku akieleza kwa sasa mkoa wa Tanga inafanyika kwa kuanzia vyama vya ushirika vya wafugaji ambao vikifanya vizuri zaidi vitasaidia vyama vyengine kufikika kwa urahisi zaidi.

 

“Lakini nitoe wito kwa vyama vya ushirika na viongozi mliopata mkopo lakini lazima mtambue kwamba marejesho yake ni kupitia zile shughuli ambazo wanaushirika wanazifanya kila siku ”Alisisitiza .

 

Mrajisi huyo alisema iwapo mkopo huo ukiendelea vizuri na wakiendelea kufanya ushirikiano mzuri wataendelea kufungua wigo mpana kwa vyama vyengine vya ushirika vya mchepuo mwengine kuweza kunufaika nao.

 

Hata hivyo kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union (TDCU) Athumani Mahadhi alisema chama hicho kilianzishwa mwaka 1993 wakiwa na lengo la kutafuta soko la wafugaji wa Ng’ombe wa maziwa mkoa wa Tanga.

 

Alisema kwea sasa wana vyama wanachama 28 na wafugaji mmoja mmoja wamefikia kwa mkoa mzima wamefikia 6285 huku akieleza katika mpango huo wa bima ya afya wao kama TDCU na vyama vya  wanaona kama itakuwa itachochea baadhi ya watu ambao sio wanachma  kuona ipo haja ya kujiunga kwenye vyama vya ushirika kutokana na kwamba huduma ya afya pia inapatikana huko.

 

No comments:

Post a Comment

Pages