HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 07, 2021

Prof. Joyce Ndalichako afanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia

 


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (katikati), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia ukanda wa Afrika, Dk. Taufila Nyamadzabo (kushoto), leo Juni 7, 2021 Jijini Dodoma.

 

 

Picha ya kumbukumbu.


Na Mwandishi Wetu

 

Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, leo Juni 7, 2021 Jijini Dodoma amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia ukanda wa Afrika, Dkt Taufila Nyamadzabo kuzungumzia utekelezaji wa miradi ya elimu inayofadhiliwa na Benki ya Dunia Nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu pia amehudhuri kikao hicho.

Baadhi ya miradi iliyojadiliwa ni Mradi mpya wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP)  ambao unalenga katika kuimarisha Elimu ya Sekondari nchini ikiwa ni pamoja na kuongeza nafasi zaidi kwa kujenga shule zaidi ya 1000, maendeleo ya Mradi wa EP4R, miradi inayolenga  kuboresha Elimu ya Juu Nchini ikiwemo Mradi wa Kuboresha Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET) na Mradi wa Kukuza Ujuzi na Stadi za Kazi (ESPJ).

No comments:

Post a Comment

Pages