HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 14, 2021

TET, UNESCO yawafunda walimu somo la Stadi za Maisha




Na Mwandishi Wetu

TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni  (UNESCO) inaendesha mafunzo ya ujaribishaji wa miongozo ya elimu ya stadi za Maisha kwa walimu  wa shule za Msingi  na Sekondari nchini.

Akifungua mafunzo hayo katika wilaya ya Temeke, Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala (TET) Bi. Fika Mwakabungu amesema kuwa, walimu  1696 katika halmashauri 13 nchini watapatiwa mafunzo hayo na kisha wataweza kuwafundisha wenzao ili wakatoe uelewa wa stadi za maisha.

"Karne hii  ya 21 wanafunzi wanapaswa kuandaliwa mapema kwani wanakutana na mambo mengi hivyo tunapowaandaa mapema kujua masuala mbali mbali wataweza kuepukana na changamoto" alisema Bi Fika.

Mafunzo hayo ya stadi za maisha yanahusisha masuala ya afya,afya ya uzazi,Vvu na ukimwi na jinsia na namna ya kuondokana na ukatili  wa kijinsia.

Kwa upande  wake,mwezeshaji wa mafunzo hayo ,Bi.Amina Tou ameeleza kuwa,wana imani walimu wanaohudhuria mafunzo hayo wataweza kuwaelimisha wengine katika shule zao ambapo pia watahakikisha kwamba wanafunzi watakaopewa elimu hiyo iwasaidie.

Mafunzo hayo  yameanza kufanyika leo katika halmashauri 13 ambazo ni; Ilala, Temeke, Ngorongoro, Ifakara, Kasulu, Kisarawe, Kibondo, Ulanga ,Morogoro mjini,Malinyi,Sengerema,Bagamoyo na Mlimba.

No comments:

Post a Comment

Pages