HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 07, 2021

"UKIONA DAWA YA ANTIBIOTIKI UKIENDA HAJA NDOGO HAITOI HARUFU HIYO NI BANDIA"- TMDA


Na Mwandishi Wetu, Kibaha

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Nchini (TMDA), Bw. Adam Fimbo ameitaka Jamii kuwa watambuzi  kwenye kuzingatia dawa halisi ama bandia kwa dawa za Antibiotiki hasa matokeo ya dawa hizo wanazotumia kuwa na viashiria ikiwemo harufu kwa mkojo.

Fimbo amesema hayo wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku Nne (4) kwa Wakaguzi 59 wapya kutoka Kanda Nane (8) za Mamlaka hiyo yanayofanyika mjini hapa, Kibaha Mkoani Pwani alisema

Ambapo alibainisha kuwa  TMDA wanakuwa na utaratibu wa mafunzo hayo mara kwa mara ilikuwajengea uwezo wakaguzi ilikuzuia mianya ya kuingiza dawq bandia ama zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu.

Ametoa rai kwa jamii kutambua dawa zote za Antibiotic endapo watazitumia lazima ile harufu ya dawa hiyo baada ya kutumia itatoa harufu katika mkojo wa mtumiaji.

"Kama hutasikia harufu katika dawa hiyo ujue hakuna dawa humo." Alisema Fimbo kwa kusisitiza jamii kutambua hilo.

Pia ameongeza kuwa, kwa upande wa dawa za wajawazito za kuongeza damu za Iron (foric acid) , lazima baada ya kutumia dawa hizo kinyesi chake kiwe cheusi kuashiria ni dawa sahihi.

"Kinyesi kisipokuwa cheusi ujue hamna dawa humo ndani ya hiyo dawa. Kila dawa inamatokeo yake baada ya kutumia lakini isipotoa matokeo husika ujue dawa hiyo ni bandia hivyo inatakiwa hatua kuchukuliwa haraka". Alisema Fimbo.

Aidha aliongeza kuwa, dawa zote zilizosajiliwa ama  zilizokaguliwa na TMDA zinatakiwa kuwa na namba za TMDA za usajiri ili kuwahakikishia watumiaji ubora na viwango vilivyokusudiwa katika matumizi hata hivyo mtumiaji lazima achukue taadhari ya dawa anayotumia kama ni sahihi au ni bandia.

Fimbo alisema mwananchi akague nembo maalumu ya usajiri kutoka TMDA katika kila dawa anayonunua ilikujiridhisha kama ni salama ili kuepuka kutumia dawa bandia na kupata madhara.

"Dawa zilizosajiliwa na TMDA zina nembo inayoanzia na TZ na nembo ya dawa inayoanzia na TZA ambapo kila unapoangalia lebo ya dawa utaona namba hizo ambazo zitakuhakikishia kwamba dawa hiyo imesajiliwa na TMDA". Alisema Fimbo.

Aliongeza kuwa: Dawa inapaswa ikuponye na iwapo unatumia dawa kwa muda ulioandikiwa lakini hukupona hiyo ni dawa bandia.

Katika mafunzo hayo, pia amewataka Wakaguzi  hao wapya kujiadhari na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa kwani mamlaka hiyo imekuwa ikisimamia haki katika kulinda afya za jamii hivyo hakuna kupokea wala kutoa rushwa.

"Sekta ya dawa inavishawishi vikubwa kwa wadau wake ikiwemo vitendo vya rushwa kwakuwa nyinyi ni Wakaguzi wapya muende mkazingatie maadili ya utumishi ikiwemo kuepuka vitendo vya rushwa.

"Mkiruhusu dawa kwa vitendo vya rushwa tutabaini tu kwani matumizi ya dawa yanachukua muda mrefu na bahati nzuri wafanyabiashara ukiwabana wanataja, sasa mzingatie maadili ya nchi nyinyi ni muhimu sana kulikokupitisha dawa bandia itasababisha madhara makubwa kwa jamii na kutia aibu kwa taifa". Alimalizia Fimbo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TMDA,  anayeshughulikia dawa na vifaa tiba Dkt. Yonah Mwalwisi amesema mamlaka hiyo inatumia mbinu na mifumo mbali mbali inayosaidia ya kudhibiti ubora katika soko la nchi kwa kuhakikisha linapata vitendanishi na vifaa vyenye ubora, salama na vyenye ufanisi unaotakiwa.


"TMDA tunatumia mifumo ya kisasa ya kielectroniki ambayo hutumika  kuthibiti wakati wa kuingiza vifaa tiba au vitendanishi nchini kwa mteja wa bidhaa husika kutoka taifa analotaka kisha hukaguliwa kwa lengo la kujiridhisha ubora wa kifaa husika." Alisema Mwalwisi.

Mafunzo hayo ya siku Nne, yameanza leo ambapo wakaguzi hao watapatiwa mafunzo ya nadharia na kwa vitendo na yanatarajiwa kufungwa 10 Juni mwaka huu.

TMDA imeandaa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani [WHO] amabapo mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na kila mwaka kwa wakaguzi na maafisa wa TMDA.

No comments:

Post a Comment

Pages