HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 07, 2021

UVUNAJI MALIASILI ENEO TENGEFU WATAKIWA KUWA ENDELEVU

 


 

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

MALIASILI ni moja kati ya vyanzo vimekuwa vinavyosabaisha uchumi wa nchi au Taifa husika kunufaika.

Kufuatia hali hiyo, uvunaji wa maliasili katika eneo tengefu unatakiwa uwe endelevu ili uweze  kunufaisha mazingira pamoja na binadamu na pasiwe na migogoro kati ya mazingira na binadamu.

Ni kauli ya Mkuu wa Kitengo Sayansi Asilia Kelvin Robart kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Sayansi na utamaduni kwenye mahojiano maalum na kuongeza kwamba, kuna maliasili za aina mbalimbali zinazoweza kusaidia maendeleo katika nchi

"Sisi kama UNESCO tunahamasisha masuala mazima ya uhifadhi wa Mazingira na maliasili kwenye maeneo tengefu kwa kuhakikisha maeneo yote ambayo  yametengwa hayaingiliwi na  shughuli za Watu au kusababisha migogoro na wananchi au wakazi wa eneo husika.

 KUHUSU FAIDA
Amesema maeneo tengefu yanafaida katika nchi kwani huleta  pesa  kutoka kwa wadau mbalimbali wanao uhifadhi kwenye gazi za Kimataifa.

"Ni kweli maeneo hayo yanafaida kwa sababu UNESCO ni shirika la umoja wa Mataifa hivyo eneo likitambulika kama ni tengefu nchi inanufaika na inakuwa ni rahisi kupata fedha kwaajili ya uhifadhi kutoka maeneo mbalimbali.

Na kuongeza kuwa, "Nchi kunufaika na maeneo hayo kwa kutangazwa kidunia kwasababu kunamtandao wa sehemu tengefu ambapo unaweza kujulikana duniani kote," amesema Mkuu Huyo.

CHANAGMOTO ZENYEWE ZINASEMAJE?
Aidha amesema changomoto kubwa wanayokabiliana nayo ni masuala ya uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za binadamu ambao wamekuwa wakivuna rasilimali ili weweze kujikimu kwa maisha yao ya kila badala ya uvunaji endelevu.

"Na ndio Maana umekuwa tukifanya Kazi na Taasisi za Serikali na wadau mbalimbali Ili watusaidie uvunaji unaofanywa na wananchi uweze kuwa endelevu," amesema Robart.

Ameeleza changamoto nyingine ni mabadiliko ya tabia ya nchi imebadilisha hali ya mvua na kusababisha tatizo la  ukame ambapo Baadhi ya wananchi waliokuwa wanalima sehemu zao kuamua kwenye maeneo tengefu.

"Kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na mvua zisizo eleweka wananchi wamekuwa wakilima maeneo yaliotengwa hii ninchanagoto kubwa kwetu," amesema.

TAFSIRI YA SAYANSI ASILIA
Ni masuala yote ya mali asili katika Sekta  ya Sayansi Asilia  ambapo inajumuisha  Sayansi ya maji, ikorojia,Sayansi ya Dunia,madini gesi na masuala ya majanga,
Hata hivyo amesema mpango wao wa kusimamia maeneo tengefu wanashirikiana na NEMC ,Ofisi ya Makamu wa rais,Wizara ya Maliasili pamoja na Utalii,Ngorogoro.

Amesema lengo kubwa la kufanya kwenye maeneo hayo tengefu ni kuhakikisha maeneo hayo yanaifadhiwa Ili yaweze kuwanaufaisha wananchi wote waliopo karibu na  maeneo hayo.

'Ili eneo lionekano ni tengefu basi eneo hilo linatakiwa lisiwe na mgogoro wa wa aina yoyote nandio Maana sio kila eneo ni eneo tengefu.

Ameyataja maeneo hayo tengefu kuwa ni Gombe masito ugala, East usabara,Lake Manyara,Jozwani jagwabei lililopo kisiwani Zanzibar na Ngorogoro, Serengeti.

Shughuli kubwa ya UNESCO nikuwajengea uwezo Taasisi pamoja na wadau wanao shiriki wanaosimamia usimamizi masuala ya Mazingira lengo ni kuwa na amani kati ya mazingira na binadamu.

No comments:

Post a Comment

Pages