Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa tatizo la matumizi ya Dawa za kulevya Nchini limeendelea kuongezeka siku hadi siku huku akitoa Maelekezo mbalimbali kwa wadau katika kuwasiadia waathirika wa dawa za kulevya kiuchumi ili wasirudi katika matumizi ya Dawa hizo.
Maelekezo hayo yametolewa hii leo Jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene kwaniaba ya Waziri Mkuu katika Maadhimisho ya Kilele Cha siku ya mapambano ya Dawa za kulevya ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Dodoma.
Sanjari na hilo ametaka kuangaliwa kwa mitaaala ya Elimu kwa kuongeza somo la dawa za kulevya ili kuweza kuliokoa kundi la Vijana ambalo lipo hatarini katika matumizi ya Dawa za kulevya.
Awali akitoa taarifa kuhusiana na mapambano ya Dawa za kulevya, Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kuzuia na kupambana na Dawa za kulevya Nchini, Gerald Kusaya ameeleza jitihada zinazofanywa na Mamlaka hiyo huku akieleza changamoto zinzazowakabili.
Kwa upande wao Wadau wa maendeleo akiwemo Balozi wa Italia Nchini Tanzania, Marko Lombadi, John Mark ambaye ni mpelelezi kitengo cha kupambana na Dawa za kulevya wa Umoja wa Nchi za ulaya UK wakeleza athari za madawa ya kulevya na kuahidi kushirikiana na Serikali katika mapambano ya Dawa za kulevya ili kuweza kutokomeza matumizi ya Dawa hizo ambazo zimekuwa na athari kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Nao baadhi ya Waraibu wa Dawa za kulevya walikuwa na haya ya kusema.
Maadhimisho hayo yalianza rasmi Juni 23 ambapo Kilele chale kimehitimishwa Juni26 yakibebwa na kauli mbiu isemayo "Tuelimishane kuhusu tatizo la Dawa za kulevya kuokoa Maisha.
June 29, 2021
Home
Unlabelled
Wadau watakiwa kuwasaidia kiuchumi waathirika wa dawa za kulevya
Wadau watakiwa kuwasaidia kiuchumi waathirika wa dawa za kulevya
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment