HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 15, 2021

WANASHERIA WATAKIWA KUJIELIMISHA

 


Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


MWANASHERIA  Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, amewataka Mawakili wa Serikali Nchini kuendelea kujielimisha kila siku kutokana na kukua kwa taaluma ya Sheria Ulimwenguni  kulingana na umuhimu wa kazi yao wanayoifanya ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.
 
Profesa Kilangi ametoa wito huo  leo Jijini Dodoma  wakati akifungua mafunzo ya siku nne kwa Mawakili wa Serikali yenye lengo  la kuwaongezea uwezo katika stadi za uendeshaji madai ya usuluhishi kwa kuwapa ujuzi ambayo yameandaliwa na  Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Amebainisha kuwa  mafunzo hayo ni muhimu na yatasaidia kuwanoa Mawakili hao ili kuendana na mabadiliko ya taaluma ya Sheria ambayo yamekuwa yanatokea kila siku ulimwenguni.


Sambamba na hilo amesema Mafunzo hayo yataongeza uwezo na weledi katika suala zima la usuluhishi la madai mbalimbali huku akiitaka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kushirikiana na Taasisi mbalimbali katika kutatua changamoto  mbalimbali zinazoikabili  ofisi hiyo  ikiwemo uhaba wa mawakili wa Serikali.

 

Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali,Gabriel Malata amesema ofisi hiyo ilipewa jukumu lakuendesha madai ya kesi ndani nan je ya nchi na kupitia mafunzo hayo yanaenda kuwaweka katika mtazamo mmoja wa uendeshaji wa mashauri kwaniaba ya Serikali na Taasisi zake huku akibainisha mafanikio na changamoto mbalimbali.
 

No comments:

Post a Comment

Pages