HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 13, 2021

AZAKI KUKUTANA JIJINI DODOMA

 Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

Jumla Asasi za kiraia 1500 zinatarajia kukutana katika wiki ya Asasi za kiraia (AZAKI),  inayotarajiwa kuanza kufanyika oktoba 23 hadi 29  mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Akizungumza kwa   niaba ya kamati ya maandalizi  leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma  ,mwenyekiti  wa kamati hiyo ,Mkurugenzi mtendaji   wa asasi ya Hakirasilimali  Rachel  Chaganja amesema lengo la  wiki hiyo ni kuendelea kuimarisha na kujenga mahusiano mazuri baina ya  serikali,watu binafsi pamoja na Asasi za kiraia katika ujenzi wa taifa ambapo takribani asasi  1500 pamoja na zaidi ya watu 4000 watashiriki.

Aidha ameeleza kuwa katika  wiki hiyo kutakuwepo na mijadala na midahalo mbalimbali  pomoja na maonyesho ya kazi  zinazofanywa na Asasi za kiraia  Kama Msaada wa masuala ya kisheria.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji kutoka shirika la CBM, amesema kutakuwa na utoaji wa tuzo Kwa mashirika na taasisi ambazo zimekuwa na mchango mkubwa Kwa serikali na tuzo Kwa vyombo vya habari .

 Naye Mkurugenzi  mtendaji kutoka  asasi ya kiraia ya  Foundation for civil society [FCS],FRANCIS KIWANGA, amesema wiki hiyo  ya asasi za kiraia itachochea Kubadili mtazamo Kwa wananchi  na kutambua umuhimu wa Asasi za kiraia.

Akizungumza kwa  niaba ya serikali mwakilishi wa msajili wa Asasi za kiraia kutoka wizara ya afya Maendeleo ya Jamii Jinsia ,Wazee na Watoto  FAKI  SHARIB, amesema jukumu la serikali ni kuweka mazingira wezeshi Kwa Asasi za kiraia Kwa kufanya kazi Kwa kuzingatia  Sheria na kanuni zilizowekwa.

No comments:

Post a Comment

Pages