HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 20, 2021

Dk. Akwilapo: TESP itaboresha zaidi elimu

Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo akizungumza na wanahabari muda mfupi baada ya kufungua mkutano wa wadau wa elimu waliotathimini nusu ya kwanza ya mradi wa kuboresha.
Mwakilishi kutoka serikali ya Canada akizungumza na wanahabari muda mfupi baada ya uzinduzi wa mkutano wa kutathimini nusu ya kwanza ya mradi wa TESP uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

 


Na Irene Mark

SERIKALI imesema itaendelea kuwekeza kwenye miradi ya kuandaa na kupata walimu bora ili kutokomeza maadui watatu wa taifa hili waliopo tangu uhuru.

Kauli hiyo ya serikali ilitolewa jijini Dar es Salaam leo Agosti 20,2021 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo alipofungua mkutano wa kutathimini nusu ya kwanza ya mradi wa kuboresha Mafunzo ya Ualimu Tanzania (TESP), unafadhiliwa na seriakali ya Canada.

Katika mkutano huo wa siku mbili uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu, Dk. Akwilapo amesema mafanikio ya TESP, yanaongeza mwanga wa matumaini kwenye sekta ya elimu hasa kwa kupata walimu bora wanaokwenda sawa na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano.

“Hili taifa lina maadau watatu ujinga, umaskini na maradhi, sasa tunapambana na ujinga ambao ukiondoka maradhi yataisha na umaskini utaondoka.

“Mradi huu wa miaka mitano unawaandaa walimu kuwa ‘compitent’ sasa ukiwa na mwalimu bora na mwenye ujuzi una uhakika wa kumpata mwanafunzi bora,” amesema Dk. Akwilapo.

Kwa mujibu wa Dk. Akwilapo, zaidi ya Sh. bilioni 84 zilizotolewa na Serikali ya Canada zinatumika vema kuhakikisha miundombinu ya vyuo vya ualimu na njia za ufundishaji zinaboreshwa ili kwenda na wakati kwa ajili ya kupata walimu bora.

Amesema kupitia mradi huo vyuo sita vimejengewa   maktaba, vingine maabara na kujenga chuo kipya cha elimu kilichopo Kabanga.

Mwakilishi kutoka Serikali ya Canada, Hellen Fytche amesema nchi hiyo itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kutekeleza miradi yenye tija kwa maendeleo.

“Tupo tayari kushirikiana na serikali hii sikivu kwenye miradi ya maendeleo kwa sekta ya Elimu, Afya na Mazingira,” amesisitiza Fytche.

No comments:

Post a Comment

Pages