Na Lydia Lugakila, Bukoba
Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Muleba mkoani Kagera inawashikilia watu 20 waliokuwa wanajihusisha na uvuvi haramu katika Ziwa victoria pamoja na nyavu aina ya timba vipande16 zenye urefu mita 1600 pamoja na Pikipiki tatu.
Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Toba Nguvila, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Muleba amesema kuwa watu hao wote ni wakazi wa kata ya Kagoma ambapo walikuwa wanavua samaki zisizokidhi vigezo majira ya usiku kwa kutumia nyavu hizo aina ya timba.
Nguvila amesema kuwa baada ya kuunda kikosi kazi cha kudhibiti uvuvi haramu katika ziwa victoria wameendelea kubaini mtandao wa watu wanaojihusisha na uvuvi haramu kwani Kati ya watu hao 20 watengenezaji wa hizo timba ni 6 na vijana 14 ambao walikuwa wakivua samaki kwa kutumia nyavu hizo.
Naye Afisa Uvuvi Wilaya ya Muleba, Wilfred Tibendelana, amesema moja ya madhara ya nyavu hizo ni kutooza pindi zinapokuwa zimazamishwa majini na zinaendelea kukamata mazalia ya samaki hivyo ameshukuru kamati ya ulinzi na usalama kwa kuunda kikosi kazi cha kudhibiti uvuvi usiokubalika kisheria kutokana na zoezi hilo ni endelevu ili kuweza kulinda rasilimali za ziwa victoria.
Aidha watuhumiwa hao 20 wanatarajia kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu mashitaka yanayo wakabili.
No comments:
Post a Comment