KLABU ya Soka ya Azam FC imemtambulisha Dkt. Jonas Tiboroha kuwa
Mkurugenzi Mpya wa Masuala yote ya Mpira 'Soka' pamoja na kuzindua Kauli
Mbiu ya Msimu kwa 2021/22 isemayo Azam FC: Kimya Kimya ikiwa zimepita
siku mbili baada ya kuzindua nembo mpya ya klabu hiyo.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
KLABU
ya Soka ya Azam FC imemtambulisha Dkt. Jonas Tiboroha kuwa Mkurugenzi
Mpya wa Masuala yote ya Mpira 'Soka' pamoja na kuzindua Kauli Mbiu ya
Msimu kwa 2021/22 isemayo Azam FC: Kimya Kimya ikiwa zimepita siku mbili
baada ya kuzindua nembo mpya ya klabu hiyo.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam katika Hafla ya utambulisho huo,
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' amesema
wameamua kumpa nafasi hiyo Dkt. Tiboroha kutokana na uzoefu alionao
katika masuala ya soka na kwamba wanategemea kuifikisha klabu hiyo
mbali.
" Tumeamua kumtabulisha Dkt. Jonas kuwa
mkurugenzi wa masuala yote ya mpira wa klabu yetu kwa uzoefu wake
tunategemea atatusaidia kutimiza malengo iliyojiwekea, " amesema Popat.
Amebainisha
kuwa kwa muda mrefu watu wanamtambua yeye CEO pekee wa klabu hiyo
pamoja na watendaji wengine hivyo wamemtambulisha Dkt. Tiboroha
kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja lengo likiwa kuisaidia
timu hiyo kufikia malengo na kuendelea kuwa imara na kuiboresha timu
hiyo.
Kwa upande wake Dkt. Tiboroha
ameishukuru klabu hiyo n uongozi mzima kwa kumwamini kumpatia nafasi
hiyo hivyo anajiona mwenye bahati na kwamba ana deni kubwa la kuifanyia
Azam FC.
Amefafanua kuwa atahakikisha
anaisaidia klabu hiyo kutimiza malengo yaliyowekwa na klabu yanafikiwa
kwa kuangalia majukumu yote yaliyomo kwenye mpango kazi.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa klabu hiyo, Thabit Zacharia 'Zaka za
Kazi' amesema baada ya uzinduzi wa nembo ya klabu hiyo wameamua kuja na
kauli mbiu hiyo kwano msimu ujao mambo yao yatafanyika kimya kimya.
No comments:
Post a Comment