HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 17, 2021

METHEW AVIPIGA JEKI VIFAA MICHEZO KLABU 14 KATA ZA MTAMA, MAJENGO



 

Na Mwandishi Wetu

 

KATIKA kuhakikisha Michezo inaendelea kusonga mbele hapa nchini,wadau wameombwa kujitokeza kuzisaidia vilabu vya chini katika Halmashauri mbalimbali,ikiwemo ya Mtama,ili kuibua vipaji kwa vijana,wakiwemo wa kiume na wanawake katika Halmashauri yao.

Wito huo umetolewa na mdau Selemani Methew wakati anakabidhi vifaa mbalimbali vya Michezo vyathamani ya Sh,4.800,000/-kwa vilabu 14 vya Mpira wa Miguu,Mikono (Pete),Volball na Filimbi kwa kata za Mtama,Nyangao na Majengo.

Vilabu vilivyofanikiwa kupata msaada huo ni pamoja na waendesha pikipiki na Bajaji (Bodaboda FC),Majengo FC,Nyangao FC,Lima FC, Mbagala FC,Mkwajuni FC,Mtama FC,Nyengedi FC,wakati Sekondari ni Mahiwa na Mtama na zile za msingi ni majengo na Nyangao kila moja zimepata Jezi,mpira mmoja na Filimbi.

Klabu za mpira wa mikono za Mtama Veterani na Dada’s zikiwemo za Shule za msingi Nyangao,Mtama kila moja zimezawadiwa Jezi seti moja na Mpira na Filimbi,huku walimu wa michezo wakiambulia Jezi pea moja na Ofisi ya Utamaduni Halmashauri ya Mtama ikikabidhiwa Nyavu za magoli na mpira wa Volball.

Luhongo akikabidhi vifaa msaada huo,Luhongo amesema lengo la kugawa vifaa hivyo ni kuibua vipaji kwa vijana na kukuza Michezo kwa vilabu vilivyopo Halmashauri ya Mtama,ili timu ziweze kushiriki Ligi kuu na mashindano mengine.

“Mimi kwa vile nimewahi kucheza mpira naujuwa faida zake,hivyo nimeamua kusaidia ndugu zangu vifaa vya michezo”Alisema Luhongo.

Mdau huyo masuala ya Michezo amewasisitiza viongozi wa vilabu vilivyopewa msaada huo kuhakikisha wanatunza vifaa hivyo ili viweze kuchukuwa muda mrefu kuitumia.

Mohamedi Issa kiongozi wa Klabu ya Bodaboda, Mwanajuma Selemani (Veterani) na mwalimu Julieta Michael wakizungumza kwa niaba ya Vilabu vingine,wamemshukuru mdau Luhongo kwa msaada aliowapatia kwani vifaa hivyo utasaidia kuendeleza michezo ndani ya Halmashauri ya Mtama.

Katika hafla ya kukabidhiwa kwa vifaa hivyo ilitanguliwa na michezo mbalimbali,ikiwemo kufukuza kuku,kukimbia na yai kutumia vijiko,kutunga uzi kwenye sindano,kukimbia ndani ya magunia na kucheza mpira wa wavu na pete,ambapo timu ya Dada’s iliibuka mshindi kwa kuilaza Veterani magoli 14 kwa 12.

No comments:

Post a Comment

Pages