Mkurugenzi Mtendaji wa JATU PLC akiwatangazia wanachama matokeo ya hisa zilizouzwa katika Mkutano Mkuu wa Kilimo wa Wakulima wa JATU PLC uliofanyika jijin Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa JATU.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Kampuni
ya Umma inayojihusisha na kilimo, masoko na mikopo ya JATU PLC
imetangaza matokeo ya hisa za milioni 15 ilizoziweka sokoni huku
ikibainisha hisa hizo zimefanikiwa kuleta jumla ya Sh Bilioni 7.5 kwa
kila hisa moja iliyokuwa ikiuzwa Sh 500.
Matokeo
hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo Peter Gasaya katika Mkutano Mkuu wa Wakulima wa JATU PLC
uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ubungo Plaza jijini humo.
Amesema
kampuni hiyo ilifanikiwa kuuza hisa milioni 155,263,372 na kupata Sh
Bilioni 7.5 mabayo ni sawa na asilimia 104% ambapo malengo waliyojiwekea
na kusisitiza kuvuka asilimia 4% ya walichokitegemea.
"
Tuliingia soko la hisa tukauza hisa milion15 kilichopatikana ni Sh
bilioni 7.5 pesa ilienda kuwekeza kwenye Mradi wa Kilimo Kiteto mkoani
Manyara kinachofanyika kwa umwagiliaji wa kisasa, msimu huu tunaongeza
zao la ngano," amesema Gasaya.
Amebainisha kuwa
watu wasio Watanzania walionunua hisa hizo hawazidi watano na kwamba
asilimia 99% walionunua hisa hizo ni wawekezaji watanzania na kusema
wamepata wawekezaji wapya 10,000.
Amewashauri
wakulima ambao hawajajiunga na kampuni hiyo kujiunga kwani mkulima
akijiunga anapunguza gharama za ukulima katika hatua ya mwanzo hadi
mavuno kwa kuwa JATU PLC wanamsimamia mwanachama hatua zote.
Amesisitiza
kuwa katika matokeo yaliyotangazwa wakulima waliwekeza kwenye mazao
mawili ya Mahindi na Mpunga ambapo mwaka 2019/20 wakulima kwa upande wa
zao la mahindi walikuwa 71 na kwa mwaka 2020/21 waliongezeka kufikia 489
sawa na asilimia 589% huku jumla ya mavuno yalikuwa tani 9,509.58.
Ameongeza
kuwa zao la mpunga kwa mwaka 2019/20 llilikuwa na wakulima 243 na
2020/21 walikuwa 599 sawa na 147% waliolima ekari 6,633 huku jumla ya
tani 8,755.56 zilivunwa kwa mwaka huo.
Amewaomba
watanzania kujiunga na JATU Saccos ili kuweza kukidhi vigezo vya kupata
mikopo katika taasisi za fedha na kwamba kujiunga mwanachama anatakiwa
awe na hisa angalau kwenye JATU PLC.
No comments:
Post a Comment