MKuu wa Mkoa wa Mkoa wa Pwani, Aboubakari Kunenge, akizungumza na
ndugu jamaa na marafiki alipoongoza mamia yawananchi katiba mazishi ya
msiba huo wa wanafunzi waliodariki kutokana na kupata ajali.
NA VICTOR MASANGU
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakari Kunenge amewaongoza
mamia ya wananchi kushiriki katika Mazishi ya Watoto watano waliofariki
kwenye Ajali iliyohusisha Pikipiki na Fuso Eneo la Kata ya Kimange
Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa Ameeleza kuwa Mnamo Tarehe 6
Agosti, 2021 majira ya saa 1 :15 Jioni Gari aina Mitusubish Fuso Na 198
CWN ikitokea Dar es salaam kwenda Arusha iligonga Mwendesha Pikipiki
kusababisha vifo vya Wanafunzi wanne pale pale na mmoja kufariki
akipatiwa matibabu Hospital ya Jeshi Kihangaiko.
Ameeleza
kuwa Wanafunzi hao watano wa Kimange Sekondari walikuwa wamepakiana
kwenye Pikipiki wakitokea Kimange kuelekea Mbwewe. Wanafunzi hao
walikuwa wakitokea michezoni shule jirani ya kwamakocho Sekondari.
Wanafunzi
hao waliofariki ni Laya Ubwa Masudi (16) mwanafunzi wa Kimange
Sekondari Kidato cha tatu, Furaha Athumani (16) Mwanafunzi Kimange
Sekondari Kidato cha tatu, Athumani Bushiri (15) Mwanafunzi kimange
Sekondari Kidato cha Kwanza, Amina Msomba (15) Mwanafunzi Kimange
Sekondari Kidato cha Kwanza na Athumani Mchafu (17) Mwanafunzi Kidato
cha tatu.
Ameeleza kuwa
Chanzo cha Ajali hiyo ni Uzembe wa Dereva wa Gari na mwendo kasi
uliosababisha kushindwa kumudu Gari hilo na kupelekea kumgonga
Mwendesha Pikipiki akiyekuwa mbele yake.
Amethibitisha kuwa Jeshi la polisi limefanikiwa kumshikilia Dereva wa Gari hilo kwa ajili ya hatua za kisheria,
Kunenge
ametoa pole sana kwa Familia na Wananchi wa Kata hiyo kwa Msiba Mkubwa
ambao wameupata. "Kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan nitoe
pole nyingi kwenu alisema Kunenge"
"Kubwa zaidi kwetu ilikuwa ni kuja kushiriki nanyi, tumekuja na Swadaka Ndogo kwa ajili ya kufariji familia hizi. "Yaliyotokea yametokea, niwaombe tuzingatia matumizi ya vyombo vya Moto.
Kunenge
amebainisha kuwa katika upande wa Serikali wataendele kuchukua hatua
kwa mujibu wa Sheria za nchi. Dereva wa Gari hilo tunaye tutachukua
hatua" Alisema Kunenge.
No comments:
Post a Comment