HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 21, 2021

KISHINDO CHA TAMASHA LA KUMSHUKURU MUNGU DAR


Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 21, 2021 kuhusu ujio wa tamasha la  kumshukuru Mungu litakalofanyika Oktoba 3 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwimbaji wa nyimbo za injili, Upendo Nkone na Messi Chengula.

 

Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 21, 2021 kuhusu tamasha la  kumshukuru Mungu kwa ajili ya Taifa la Tanzania litakalofanyika Oktoba 3 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwimbaji wa nyimbo za injili, Jessica Honore na Upendo Nkone.


Upendo Nkone akiimba moja ya nyimbo zake.

 

 

 Jessica Honore akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa kutambulisha kwa waandishi wa habari ujio wa tamasha la kumshukuru Mungu litakalofanyika Oktoba 3, 2021.

 

Mwimbaji wa nyimbo za injili, Messi Chengula (wa pili kulia), akizungumza wakati wa kutambulisha rasmi tamasha la kumshukuru Mungu lililoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion na kutarajiwa kufanyika Oktoba 3, 2021.katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 


Na Francis Dande, Dar es Salaam

 
KAMPUNI ya Msama Promotion imeandaa Tamasha kubwa la kumshukuru Mungu litakalofanyika Oktoba 3 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 21, 2021, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama, amesema tamasha hilo litakuwa kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Taifa la Tanzania.
 
"Mkumbuke taifa letu limepitia katika mambo mengi sana, kila mtanzania anafahamu tutaendelea kuzungumza huko mbeleni lakini  tamasha litakuwa linabeba mambo mengi, lakini tamasha lenyewe ni la kumshukuru mungu kwa ajili ya taifa letu la Tanzania." Amesema Msama.


Aidha Msama ameongeza kuwa tamasha hilo litakuwa la kihistoria kutokana na ukweli kwamba alijafanyika kwa kipindi cha zaidi ya miaka sita sasa. "Nataka niwaambie wale wanaopenda matamasha wale wapendwa wote  waliomisi matamasha ya Msama Promotion, nitafanya tamasha kubwa."

Aidha Msama amesema baada ya tamasha hilo kufanyika jijini Dar es Salaam, pia litafanyika katika mikoa nane.
 
Katika uzinduzi huo  waimbaji wa nyimbo za injili, Upendo Nkone, Jessica Honore, Messi Chengula pamoja Enock Jonas waliishukuru kwa nyakati tofauti kampuni ya Msama Promotion kwa kurejesha kwa kishindo matamasha ambayo yaliweza kutoa fursa mbalimbali zikiwemo za uponyaji.


"Tumesimama tena kwa neema ya mungu na tamasha linakuja   tarehe 3 mwezi wa kumi na mimi nitakuwepo, nawaalika watu wote  usikose, mjulishe na mwingine, mjulishe na ambaye ajui mpigie simu mwambie mambo yamekuwa mambo."Amesema Nkone.

Naye mwimbaji wa nyimbo za injili Messi Chengula, amesema "Nina kila sababu ya kumshukuru mungu kuona tena tamasha la Msama Promotion linarejea katika nchi yetu ya Tanzania kwa kweli tunaamini watu walimisi sana tamasha hili hata sisi wenyewe tulipopata mwaliko tulifurahi sana.

Kwa upande wa Jessica Honore amesema "Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya tamasha la Msama Promotion  kurudi tena ni baraka sana kwa sababu ilikuwa ni baraka kwa watu wengi sana, kuna wengine waliponywa, waliokoka, walifunguliwa kupitia tamasha hili."

No comments:

Post a Comment

Pages