Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mohamed Mwaimu akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani.
Na Lydia Lugakila, Kyerwa
Jumla ya minara 9 imeanza kujengwa wilayani Kyerwa ili kuwaondolea wananchi wilayani humo changamoto ya muda mrefu ya kutokuwa na mawasiliano.
Akizungumzia hatua hiyo katika kikao cha baraza la madiwani mkuu wa wilaya hiyo Rashid Mohamed Mwaimu amempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe, Samia Suruhu Hassan kwa kuwezesha wilaya hiyo kupata fursa ya kujengwa kwa minara 9 ya mawasiliano baada ya kuwepo kwa changamoto ya mawasiliano kuwa mbovu katika baadhi ya maeneo.
"Ndugu zangu miradi imekuja ya mawasiliano minara yetu 9 imeishaanza kujengwa ili kuhakikisha mawasiliano yanakuwa imara kitu muhimu ni ushirikiano hakika huu ni uwekezaji mkubwa" alisema mkuu wa wilaya hiyo.
Hata hivyo amezitaja kata ambazo minara hiyo inajengwa kuwa ni pamoja na Kimuli, Businde, Isingiro, Kibale, Kibingo, Kitwechenkura, Rutunguru,Songambele, pamoja na Bugomora.
No comments:
Post a Comment