HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 14, 2021

KYERWA YAPEPEA UKUSANYAJI MAPATO

 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kyerwa Bahati Enerco, akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani.

 

Na Lydia Lugakila, Kyerwa

Halmashauri ya wilaya Kyerwa Mkoani Kagera imefanikiwa kukusanya na kupokea jumla ya shilingi bilioni 25.671 sawa na asilimia 80.67.

Hayo yamebainishwa katika taarifa ya  mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyerwa Bahati Enerco katika kikao cha baraza la madiwani kwa robo ya nne 2020/2021  kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Enerco amesema kuwa halmashauri hiyo imefanikiwa pakubwa katika ukusanyaji mapato kwa kiwango cha juu huku akiishukuru serikali kupitia fedha za halmashauri na kutekeleza miradi ya maendeleo kupitia kulipa mishahara kwa watumishi na shughuli za kawaida ambapo kwa kipindi cha mwezi juni 2020-2021 hadi julai 2021 baada ya kufanikiwa kukusanya na kupokea jumla ya shilingi bilioni 25.671 sawa na asilimia 80.67 ya lengo kwa mwaka kati ya fedha hizo jumla ya shilingi bilioni  2.37 ni fedha ambazo ni mapato ya ndani zilizokusanjwa kwa asilimia 111.97 na shilingi bilioni 1.981 ya makisio ya mwaka.

Mwenyekiti huyo amewapongeza watumishi wa halmashauri pamoja na wataalam katika vitengo mbali mbali kwa ukusanyaji wa mapato na usimamizi mzuri wa fedha katika kutekeleza miradi ya maendeleo iliyoifanya wilaya hiyo inafikia katika hatua mzuri kwa muda mfupi.

Aidha kwa upande mkuu wa wilaya hiyo Rashid Mohamed Mwaimu amesema suala la ukusanyaji mapato unahitaji ushirikiano hivyo watumishi wote wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia na kukusanya mapato lengo likiwa ni kuvuka malengo zaidi ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya.

No comments:

Post a Comment

Pages