HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 19, 2021

PROF. NDALICHAKO ATAJA VIPAUMBELE VYA SH. BIL. 2.697 ZA HEET



 Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba  na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Mara Warwick, wakisaini mikataba mitano ya mikopo ya masharti nafuu kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa! (International Development Association - DA) yenye thamani ya dola za Marekani bilioni  1.167 .

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba mitano ya mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya dola za Marekani Bilioni 1.167, kutoka Benki ya Dunia kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa (International Development Association - IDA), iliyofanyika Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es Salaam leo Agosti 19, 2021.


Makatibu Wakuu wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu.


 NA MWANDISHI WETU

 
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, ameyataja maeneo ya vipaumbele, yatakayonufaika na mkopo wa masharti nafuu uliopatiwa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Dunia (WB), kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa (International Development Association - IDA).

Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia, wamesaini mikataba mitano ya mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya dola za Marekani Bilioni 1.167, kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa, ambako hafla ya utilianaji saini hizo umefanyika Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa mirada itakayonufaika kwa mkopo huo (wenye thamani sawa na Shilingi za Kitanzania Trilioni 2.697), ni pamoja na Mradi wa Kuboresha Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET), ambao uko chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mradi wa HEET unaolenga kuimarisha mazingira ya kujifunzia,  kuhakikisha maboresho makubwa ya shahada za kipaumbele ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira, sambamba na kuboresha usimamizi wa mfumo wa Elimu ya Juu chini, umetengewa kiasi cha dola milioni 425 (sawa na Sh. Bilioni 982.1).

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Ndalichako, aliyataja baadhi ya maeneo ya kipaumbele yatakayonuifaika na kiasi hicho kuwa ni pamoja na ujenzi na maboresho ya miundombinu inayozunguka elimu ya juu Tanzania.

“Kupitia kiasi hicho, wizara inatarajia kufanya mageuzi makubwa katika elimu ya juu, ikiwamo upanuzi na uongezaji wa miundombinu, ambako taasisi 23 zilizo chini ya wizara yetu zitanufaika kupitia mkopo huo wa masharti nafuu kwa Serikali.

“Mengine tunayofikiria kufanya ni ujenzi wa kumbi za mihadhara na madarasa 130, kujenga maabara na karakana 108 za kufanyia mafunzo kwa vitendo, kumbi 55 na vyumba maalum za kuendesha semina za kuwajengea uwezo wanafunzi wa elimu ya juu,” alisema Profesa Ndalichako.

No comments:

Post a Comment

Pages