HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 31, 2021

Senzo sasa ni CEO wa Mpito Yanga


 DAR ES SALAAM, TANZANIA

UONGOZI wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, umemtangaza Senzo Mbatta Mazingisa, kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mpito (Interim Chief Executive Officer), jukumu lake kuu likiwa ni kufanikisha mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo.


Kabla ya uteuzi huo, uliotangazwa Leo mchana Makao Makuu ya klabu hiyo na Makamu Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela, Senzo raia wa Afrika Kusini, alikuwa Mshauri Mkuu wa mfumo huo uliopitishwa na Mkutano Mkuu wa Yanga.


Akizungumza na wanahabari, Mwakalebela alifafanua kuwa, baada ya kufanya vema katika jukumu la awali la Mshauri Mkuu, na mapendekezo ya mfumo kurudhiwa na kupigiwa kura kwa asilimia 100 za wajumbe wa Mkutano Mkuu, uongozi umeona umkaimishe Senzo kwa jukumu la kumalizia mchakato huo, kupitia nafasi ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mpito, kama mabadiliko ya katiba yanavyotaka.


Kupitia mkutano huo na wanahabari, Senzo aliushukuru uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti Dk. Mshindo Msola kaa kuendelea kuwa na Imani naye na kwamba anaamini katika ushirikiano, hivyo kuwataka Wana Yanga kumpa sapoti Kama waliyompa akiwa Mshauri Mkuu

No comments:

Post a Comment

Pages