Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Serikali
imesema Ziara aliyoifanya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Rwanda
imeleta tija kwa kufungua fursa kwenye sekta ya elimu, usafirishaji,
uwekezaji, pamoja na viwanda huku ikibainisha ziara hiyo imeimarisha
ujirani mwema kati ya Tanzania na Rwanda na kurahisisha gharama za
usafirishaji wa bidhaa za Rwanda kupitia Bandari ya Tanga na Dar es
Salaam.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam
na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula wakati akitoa taarifa kwa wanahabari kuhusu
kilichojiri katika ziara ya ya Rais Samia aliyealikwa na Mwenyeji wake
Rais Paul Kagame.
Amesema katika ziara marais
wote walitliana sahihi mikataba ya hati za makubaliano katika maeneo
manne ikiwemo elimu, tehama, uhamiaji na usimamizi wa bidhaa za dawa na
kwamba walijadili namna ya kuwawezesha wananchi kufanya biashara kwa
pamoja na uhuru wa kuingia nchi hizi.
" Ziara
imeleta tija marais wote wametia sahihi hati za makubaliano katika sekta
ya usimamizi wa dawa wamekubaliana kuboressha bidhaa za dawa hasa
katika kipindi hiki cha janga la Corona pamoja na ujenzi wa viwanda
kufungua fursa za kibiashara," amesema Balozi Mulamula.
Amebainisha
kuwa katika sekta ya elimu Serikali ya Rwanda imeamua Lugha ya Kiswahii
kifundishwe kiingizwe katika mitaala ya shule hivyo imemuomba Rais
Samia kuipatia wataalamu wa kutengeneza mitaala na kufundisha.
Amesisitiza
kuwa akiwa nchini Rais Samia alipata fursa ya kutembelea kiwanda cha
kutengeneza magari aina ya Volkswagen na kwamba kiwanda hicho kinahitaji
soko nchini pamoja na kutemelea Kiwanda cha kutengeneza Juisi ya
Mananasi. na kwamba Rais Samia amepanga kuanzisha kiwanda hicho nchini.
Ameongeza
kuwa Rais Samia alitembelea eneo lililotokea Mauaji ya Kimbali
yaliyotokea Rwanda na kusema akifrudi nchini atahamasisha Watanzania
kutochezea amani, badala yake waimarishe umoja, mustakabali wa kisiasa
na uzalendo.
Balozi Liberata amefafanua kuwa
kupitia ziara Serikali imejifunza namna bora ya kuimarisha na kuendeleza
maeneo ya uwekezaji ili kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza katika
sekta mbalimbali.
Katika ziara ya Kiserikali
Rais Samia aliambatana n ujumbe wa viongozi wa Sekta za kimkakati
akiwemo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard
Chamuriho, Geofrey Mwambe, Saada Nkuya, Profesa Kitila Mkumbo na Dkt.
Faustine Ndungulile.
Wengine ni Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Reli nchini, Masnja Kadogosa, Msajili wa Bodi ya Maziwa,
pamoja na watendaji wa taassis nyingine za Serikali.
No comments:
Post a Comment