Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Serikali
imesema watu wanaotaka kufunga ndoa kuhakikisha wanafungishwa ndoa na
viongozi wa dini wenye vibali vya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini
Tanzania (RITA) huku ikibainisha kupitia RITA imeshasajili watoto
walio chini ya miaka mitano zaidi ya milioni sita na kufikia asilmia 55%
kutoka asilimia 13 mwaka 2012 kupitia Mpango Mkakati uliozinduliwa
mwaka 2018 hali iliyochangia kupata matokeo chanya ya kusajili watoto
wengi.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi katika Maadhimisho
ya Nne ya Siku ya Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu
Barani Afrika yanayofanyika kila mwaka Agosti 10.
Amesema
jamii inatakiwa kueewa kuwa si kila kiongozi wa dina ana ruhusa ya
kufungisha ndoa badala yake wafungishwe ndoa na viongozi waliopewa
vibali na wakala huyo huku akibainsha kupitia mpango mkakati wa usajili
huo umeleta matokeo ya kusajili watoto wengi katika mikoa ya Mara na
Simiyu ambapo ndani ya miezi minne imefikia 80% kutoka asilimia 10% za
awali.
" Si kila kiongozi wa dini anaruhusiwa
kufungisha ndoa bila idhini ya RITA hivyo ni vyema mkafungishwa na
wenye vibali, nawaomba muendelee kutoa elimu watu waone muhimu wa
kusajili vizazi, vifo, ndoa na mambo mengine mnayoyatoa," amesema Waziri
Profesa Kabudi.
Amebainisha kuwa wakala huyo
ana jukumu la kuendelea kuihamasisha jamii kuelewa umuhimu kusajili
vyeti vya matukio muhimu RITA kwani kufanya hivyo kunaisaidia Serikali
kujua takwimu halisi na kupanga mipango ya maendeleo.
Kwa
upande wake, Mwakilishi Mtendaji wa RITA ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi
wa Haki za Kisheria wa uwakala huo Lina Msanga amesema lengo la
madhimisho hayo ni kuongeza mwamko na kasi kwa wananchi kusajili
matukio muhimu ikwemo vifo, vizazi, ndoa n.k.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya RITA, Profesa Khamisi Dihenga amesema
siku hiyo hutumika kutathmini kilichofanyika katika mchakato wa usajili
wa matukio muhimu pamoja na kupoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia
kuboresha utendaji wa uwakala huo nchi nzima.
Mwakilishi
wa Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania Bi Tulia
ameishukuru RITA kwa kwashirikisha wadau mbalimbali katika maadhimisho
hayo wakiwemo viongozi wa dini, wawkilishi wa vyama vya walemavu na
Serikali huku akiongeza bado walemavu wanakabiliwa changamoto ya
miundombinu isiyo rafiki katika majengo ya umma hali inayowafnya
kushindwa kupata huduma muhimu pamoja na kunyimwa fursa za kugombea
nafasi za uongozi.
Msajili wa Usajili wa RITA
Patricia Mpuya amesema kuna umuhimu wa kusajili vizazi kwani humsaidia
mtoto kupata haki yake ya msingi ya kutambulika, kupata, kupata huduma
mbalimbali ikiwemo za kimasomo pamoja na kumlinda mtoto na ndoa za
utotoni na ajira za utotoni.na kwamba usajili wa vizazi na vifo unafanyika katika Ofisi za Makuu, Ofisi za Wilaya zote, vituo vya kata na tiba.
No comments:
Post a Comment