HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 11, 2021

KAMPUNI YA REPATRIATION ROOTS TOUR KUSHEREHEKEA UHURU WA TANZANIA BARA KWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

 


Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo, akizungumza na wadau wa Utalii jijini Dar es Salaam leo Agosti 11, 2021 kuhusu Kampuni ya Repatriation Roots Tour kuandaa tukio la kupanda Mlima Kilimanjaro Siku ya kusherehekea Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na upandaji miti 5000 kuzunguka mlima huo, lengo likiwa kuhamasisha utalii wa ndani. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Repatriation Roots Tour, Deborah Nyakisinda. (Na Mpiga Picha Wetu).


Baadhi ya wadau wa utalii wakiwa katika mkutano huo.


Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Repatriation Roots Tour, Deborah Nyakisinda, akizungumza katika mkutano wa kuhamasisha Utalii wa Ndani kwa wawakilishi wa kampuni mbalimbali  jijini Dar es Salaam leo Agosti 11, 2021. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo

 

 NA MWANDISHI WETU


Kampuni 60 zinatarajiwa kusheherekea  miaka 60 ya Uhuru kwa kupanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni juhudi zinazofanywa na Serikali pamoja na wadau mbalimbali kutangaza utalii huo nchini.

Akizungumza katika mkutano wa wadau hao Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Jaji Thomas Mihayo, alisema sekta ya utalii inapewa wa nguvu kadri siku zinavyokwenda hivyo ni muhimu kuunga mkono.

Alisema Tanzania kama ilivyo mataifa mengine imejaaliwa kuwa na vivutio vya utalii vya aina mbalimbali ukiwemo mlima Kilimanjaro pamija na mbuga za wanyama hivyo ni vyema wakatumia fursa ya uwepo wake kwenda kutembelea.

Aidha alisema utalii wa ndani ndiyo suluhisho katika masuala mbalimbali ikiwemo changamoto ya ajira sanjari na kuongeza mzunguko wa fedha nchini huku akisisitiza kuwa TTB itaendelea kuwaunga mkono wadau wote katika kuhakikisha vivutio vinatangazwa.

Kwa upande wake  Mwanzilishi wa Mpango huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya 'Repartiation Tour Roots' Deborah Nyakisinda alisema pamoja na kuutangaza Mlima Kilimanjaro, alisema tukio hilo litalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kuchangia Mtoto wa Kike kielimu, pia Afya ya Mama na Mtoto.

Alisema kuanzishwa kwa kampeni hiyo inayolenga kwenda kusheherekea kilele cha miaka 60 ya Uhuru katika kilele cha mlima huo huku akiwataka wadau wote wenye mapenzi mema kujitojeza kwa wingi ili kuunga mkono juhudi za kukuza utali wa ndani nchini.

Aidha alisema pamoja na hatua zingine sherehe hizo nitaenda sambamba na tukio la upandaji wa miti 5000 katika mlima huo ili kuboresha mazingira ya mlima huo.


No comments:

Post a Comment

Pages