HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 10, 2021

VIONGOZI ACT WAZALENDO WAWATEMBELEA WAKULIMA WA KARAFUU

Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe akiambatana na Makamo Mwenyekiti Zanzibar Ndugu Juma Duni Haji, Katibu Mkuu Ado Shaibu na viongozi mbalimbali wa Chama Zanzibar amewatembelea wakulima wa karafuu kwenye kijiji Cha Ngwachani katika Jimbo la Chambani kujionea maendeleo ya uzalishaji wa zao la karafuu.


Ziara ya viongozi hao wakiambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Ndugu Othman Masoud inaendelea leo kwenye Mikoa ya Kichama ya Mkoani na Wete. Lengo la ziara hiyo ni kufafanua maazimio ya kikao cha dharura cha Kamati Kuu kilichofanyika Unguja tarehe 08 Agosti 2021.

No comments:

Post a Comment

Pages