Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew akifunga Kikao cah kutathmini utendaji kazi kwa mwaka uliopita na kupanga mikakati ya mwaka mpya wa utendaji.
Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Mbodo.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Serikali
imewataka Viongozi wakuu wa Shirika la Posta Tanzania kuwawezesha
Mamemeja wa Mikoa wa shirika hilo vitendea kazi vya kisasa pamoja na
kuwapa uhuru wa kutekeleza majukumu yao badala ya kusubiri maamuzi
yatoke makao makuu katika utekelezaji wa majukumu ya shirika kwenye
mikoa yao.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam
na Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Mhandisi Kundo Mathew wakati akifunga rasmi Kikao cha Siku Tano cha
Kutathimini Utendaji kazi wa viongozi wa shirika hilo kwa mwaka 2020/21
na kujadili Mipango mikakati ya mwaka ujao 2021/22.
Amesema
kuwa mameneja wa mikoa wanatakiwa kupatiwa vifaa vya kisasa ili waweze
kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kwamba wasipopatiwa hawatafanya
kazi zao vizuri huku akibainisha kuwapa wigo wa uhuru katika utekelezaji
wa majukumu katika mikoa yao wajione sehemu ya maamuzi ya Posta.
"
Mameneja wapewe fursa ya kufanya maamuzi kwenye mikoa si kusubiri
yatoke Makao Makuu y Posta mkiwapa watajiona ni sehemu maamuzi ya
shirika kingine wapewe vitendea kazi vinavyoendana na mifumo ya
kidijitali posta itapata matokeo," amesema Naibu Waziri Mhandisi Mathew.
Amewataka
vongozi kwenye nafsi zao kuleta tija katika shirika hilo kwa kutekeleza
majukumu yao ipasavyo na kuingiza na kuimarisha mifumo ya utendaji kazi
iwe endelevu kwa masilahi ya shirika hilo.
Amelitaka
shirika hilo kubadilika kwa kuwaondoa viongozi wanaonekana kukwamisha
malengo posta iliyojiwekea na kukemea mabosi wanaonyanyasa wafanyakazi
hasa katika kudai masilahi yao.
Amesisitiza
mikoa ya kimkakati majiji yanahitaji kuwa na mameneja wenye uwezo
kiutendaji na kuwataka washiriki kutekeleza yote waliyoazimia katika
hicho huku akimpongeza kaimu postamasta mkuu kwa utendaji kazi bora
katika muda mfupi alivyopewa majukumu.
Kwa
upande wake Kaimu Posta Masta Mkuu, Macrice Mbodo amesema viongozi
waliohudhuria kikao hicho wamepata fursa ya kufundishwa itifaki na
maadili ya utumishi,kupitia mifumo ilyoingizwa ndani ya shirika na
kuifanya kwa vitendo, kusaini mikataba ya utendaji kazi kwa mwaka
2021/22 pamoja na kupata hekima za wazee wakongwe akiwemo aliyekuwa
Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh na PostaMasta
Mkuu Mstaafu Dus Mdeme.
Amemshukuru Naibu
Waziri Mhandisi Kundo kwa kushiriki kufunga kikao hicho na kumwaahidi
kumpa ushirikiano kwa kutekeleza yale yote waliyokubaliana kuyafanya
katika utendaji wa kazi wa mwaka 2021/22.
No comments:
Post a Comment