HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 23, 2021

Zitto kumshuhudia Hichilema akila kiapo Urais Zambia

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.
 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ameondoka nchini leo Agosti 23, 2021 kwenda Zambia kuhudhuria sherehe za kumwapisha Rais mteule wa nchi hiyo, Hakainde Hichilema.


Hakainde kutoka chama cha upinzani cha United Party for National Development (UPND) na kushinda uchaguzi huo dhidi ya Edgar Lungu wa chama tawala cha  (PF) katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni. 


Taarifa ya Naibu Katibu wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bonifasia Mapunda leo Agosti 23, 2021 kwa vyombo vya habari imesema Zitto ni mmoja wa wanasiasa wa vyama vya upinzani Afrika walioalikwa kuhudhuria sherehe hizo zinazotarajiwa kufanyika kesho Agosti 24, 2021.


Mbali na Zitto, sherehe hizo zitahudhuriwa na wakuu mbalimbali wa nchi mbalimbali akuwamo pia Rais wa Chama Kikuu cha Upinzani cha Zimbabwe Ndugu Nelson Chamisa.  


Mapunda amesema kwa muda ambao Kiongozi wa Chama hatakuwepo nchini, Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu Riziki Shahari Mngwali atakaimu nafasi ya Kiongozi wa Chama. 


"ACT Wazalendo inakitakia kila la heri chama cha UPND katika majukumu muhimu ya uongozi wa Zambia. Vilevile, Chama chetu kinamtakia Rais mteule Ndugu Hakainde Hichilema mafanikio katika majukumu yake mapya ya kuwaongoza wananchi wa Zambia." amesema Mapunda. 

No comments:

Post a Comment

Pages