Aliyekuwa Makamu wa Rais AT, John Bayo, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa Mbio za Kilimanjaro Marathon mapema mwaka huu.
NA MWANDISHI WETU
MAKAMU wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (AT), John Bayo, hatimaye amekubali yaishe na kujiuzulu nafasi hiyo bà ada ya kuandamwa kwa muda mrefu kutokuwa na sifa.
Mara bà ada ya uchaguzi mkuu wa AT mwaka jana na Bayo kuibuka kidedea yaliibuka madai kwamba hana sifa kwani moja ya vigezo ni kuwa na elimu ya Stashahada, kitu ambacho hakuwa nacho.
Licha ya madai hayo ambayo yalikuwa yamesimamiwa na wadau Johnson Maganga na Wilhelm Gidabuday, Bayo alikuwa na kigugumizi cha kuthibitisha licha ya baadaye kuwasilisha kinachodaiwa kuwa cheti chake kutoka Chuo Kikuu cha Day Star cha nchini Kenya kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambapo Baraza hilo lilidai lipo kwenye kujiridhisha.
Wakati hali ikiendelea hivyo, wadau hao walifikia hatua ya kutaka kwenda mahakamani kushinikiza uhalali wa vyeti vya Bayo uhalalishwe.
Lakini katika hali isiyotatajiwa jana, Rais wa AT, Silas Isangi, alithibitisha kupokea barua ya Bayo kujiuzulu kwa kile alichodai kuwa kutingwa na shughuli zake za kibiashara ambazo zimekiwa zikiyumba bà ada ya yeye kuingia AT.
Hata hivyo, wadau wa mchezo wa Riadha wametaka uwazi zaidi juu ya uhalali wa vyeti vya Bayo, kama kuna udanganyifu hatua za kisheria zichukuliwe na vyombo husika.
Huyu ni Kiongozi wa pili kubwaga manyanga ndani ya muda mfupi tangu uchaguzi wa AT ufanyike, mwingine akiwa Mjumbe wa Kanda ya Pwani, Robert Kalyahe.
No comments:
Post a Comment