Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leornad Akwilapo, leo tarehe 20 Septemba 2021 amepokea tuzo ya Mwanasayansi Bora katika "Plant Mutation Breeding" iliyotolewa kwa mwanasayansi mtanzania Bwana Salum Faki Hamadi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, Zanzibar .
Tuzo hiyo imetolewa na Shirika la Kimataifa la Nguvu ya Atomiki (IAEA) na kukabidhiwa Bw. Rafael Mariano Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo katika Mkutano wa masuala ya Atomiki Duniani.unaofanyika jijini Viena, Austria.
Ushindi huo umetokana na utafiti alioufanya na kuzalisha mbegu ya mpunga inayotoa Mavuno zaidi ya asilimia 60 ya mbegu za awali na ambayo inauwezo wa kuhimili ukame na magonjwa mbalimbali.
No comments:
Post a Comment