HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 20, 2021

Msajili wa Vyama vya Siasa kukutana na wadau wa siasa pamoja na Jeshi la Polisi Septemba 23


Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam kuhusu mpango wa ofisi yake kukutana na wadau wa siasa pamoja na Jeshi la Polisi Septemba 23 mwaka huu.

 

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

 OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema imeweka mpango mkakati wa kuandaa vikao vya wadau wa siasa na Jeshi la Polisi kitakachofanyika Septemba 23 mwaka huu chenye lengo la kuondoa changamoto zinazojitokeza baina yao.

Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam Msajili wa vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi amesema nia ya vikao hivyo ni kuweka mazingira rafiki na maelewano baina ya vyama vya Siasa.

Jaji Mutungi amesema kikao cha kwanza Cha wadau kitafanyika Septemba 23 ambapo ofisi hiyo itakutana na Jeshi la Polisi nchini kwa lengo la kujadili na kupata ufumbuzi juu ya malalamiko yanayotolewa na baadhi ya vyama vya Siasa katika ofisi hiyo.

Amebainisha kuwa Octoba 13 mwaka huu baraza la vyama siasa litafanya mkutano mkubwa visiwani Zanzibar ambapo utashirikisha wadau mbalimbali wa vyama vya Siasa.

“Mkutano huu utaendeshwa bila ya kuepo upendeleo kwani utaendeshwa na Waziri ambaye anamafungano ya vyama siasa ili kutia fursa kwa vyama vya Siasa kuelezea chagamoto zinazowakaba na kufikia Maridhiano”amesema 

Vikao hivi vinakuja ikiwa bado kunamalalamiko ya baadhi ya wadau wa vyama vya Siasa kushidwa kufanya mikutano yao kwa kueleza Jeshi la Polisi kuwaingilia.

No comments:

Post a Comment

Pages