Akizungumza katika tukio la ufanyaji usafi lililofanyika katika fukwe ya Mbezi jijini Dar es Salaam ikiwa ni Usafi uliofanyika kuelekea Siku ya Usafi Duniani mnamo tarehe 18 Septemba 2021, Jumamosi iliyopita Mkurugenzi Mtendaji wa Nipe Fagio, Bi. Ana Rocha alisisitiza ushiriki wa jamii na makapuni katika kutatua changamoto ya uchafuzi wa mazingira hususani utokanao na plastiki zitumikazo mara moja nchini.
“Hatuwezi kuwa na afya nzuri au maisha bora ikiwa tunaishi na uchafu, muhimu sana watu kujali mazingira na udhibiti taka Tanzania na wananchi waache kutumia mito kama madampo ya kutupia taka,” alisema Bi. Rocha.
Zoezi la kuzitambua taka likiendelea.
Mwanamuziki wa bongo fleva ambaye pia ni balozi wa mazingira, Benny Paul, akihamasisha watu kufanya usafi katika fukwe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Nipe Fagio, Bi. Ana Rocha akisisitiza ushiriki wa jamii na makapuni katika kutatua changamoto ya uchafuzi wa mazingira wakati wa tukio la ufanyaji usafi lililofanyika katika fukwe ya Mbezi jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment