Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
Serikali
kwa ushirikiano na wadau wake wa maendeleo katika Sekta ya uvuvi
inakusudia kupambana na mojawapo ya changamoto za upotevu wa mazao
yanayotokana na uvuvi ambayo yanafikia asilimia arobaini kabla ya kufika
kwa mlaji.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu
Mkuu wa wizara ya Mifugo na uvuvi , Mkurugenzi wa ukuzaji viumbe maji,
Dkt Nazael Madalla amewaambia wadau wa sekta ya uvuzi katika Ziwa
Tanganyika kuwa mradi wa FISH4ACP unaotekelezwa katika nchi 12 za
Africa, Caribbean na Pacific unalenga kukabili changamoto za upotevu wa
mazao ya samaki kabla na baada ya shughuli za uvuvi, wakati wa
uchakataji wa samaki na wakati wa kusafirishwa kwenda kwenye masoko ya
ndani na nje ya nchi.
Katika mkutano wa wadau wa
uvuvi uliolenga kujadili na kuthibitisha matokeo ya utafiti wa mnyororo
wa thamani wa dagaa na migebuka katika Ziwa Tanganyika na kubainisha
changamoto wanazokabiliana nazo, Dk Madalla amesema hatua hiyo
itasaidia kuongeza thamani ya mazao hayo katika shughuli za uvuvi
kuanzia hatua za mwanzo kutoka kwa mvuvi hadi samaki wanapofikishwa
mezani kwa hatua ya mwisho ya mlaji.
Amesema
miongoni mwa hatua zinazotarajiwa kuboreshwa katika mnyororo wa thamani,
ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kunzisha viwanda vya uchakataji,
kuinua hali ya maisha ya mvuvi kwa njia ya mikopo nafuu ili kuboresha
zana za uvuvi, kuboresha miundombinu ya usafirishaji samaki, kujenga
ushindani wa kibiashara kwa kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa
aina zote.
Dk Madalla amesema dagaa ndio
mazao yanayopotea zaidi kwa asilimia 40 hasa kipindi cha mvua kutokana
na kutegemea jua katika ukaukaji wake ili ziweze kwenda sokoni.
Katika
mchango wao,Wadau sekta ya uvuvi walipata fursa ya kupitia taarifa za
awali za matokeo ya utafiti, kujadili na kuthibitisha matokeo ya utafiti
huo unaolenga kufahamu kwa undani fursa, changamoto na hatua za msingi
za kuanza utekelezaji wa mradi huo mkubwa katika kipindi cha miaka minne
kuanzia mwakani.
Wadau wa Uvuvi wameiomba
serikali pamoja na wadau wake wa maendeleo kuharakisha utekelezaji wa
mradi huo ambao itasaidia kuondokana na changamoto zinazowakabili.
"
Tunachangamoto mbalimbali zinazotukabili kama wavuvi na wafanyabiasha,
masoko ni tatizo lakini pia hatuna mialo ya kuanikia mazao yetu kama
dagaa ndio maana hatuwezi kupata bidhaa bora ukilinganisha na maeneo
mengine,"amesema Francis John.
Mfanyabiashara wa
mazao ya uvuvi katika mwalo wa Kibirizi, Kigoma Said Idd Alli lito
shukrani kwa Serikali kuja na mradi wa ukombozi kwa wavuvi wa hali ya
chini unaolenga kuinua hali ya kipato cha mvumi kwa kutuwezesh kupata
masoko ya mazao ya uvuvi ndani na nje ya nchi, kuboresha zana za uvuvi
na hivyo kutuvusha hatua moja kwenda nyingine, “Mvuvi katika Ziwa
Tanganyika anavua hadi anazeeka akiwa na hali duni ya maisha kutokana na
kazi ya hasara misimu yote ya mvua,”
Suzana
Ezekiel ni mvuvi katika mwalo wa Kibirizi anaunga mkono hatua za
ushirikishwaji wavuvi wadogo huku akiamini hatua hiyo italeta ukombozi
kwa wavuvi wadogo. “Hakuna mvumvi wa Ziwa Tanganyika mwenye maisha
mazuri hata ukiwa na mtaji mkubwa. Kila mara changamoto zinakwamisha
maendeleo ya kazi za uvuvi. Jambo hilo linasababisha wazazi kushindwa
kulipia hata ada za shule kwa watoto wetu.”
Kwa
upande wake Mtaalam wa uvuvi kutoka FAO, Hashim Muumin amesema mojawapo
ya malengo ya mradi huo ni kuimarisha lishe kwa wananchi wa
wanaozunguka ziwa Tanganyika ili kuondokana na tatizo la utapiamlo
katika jamii. amesema wanaenda kufanyia kazi maoni ya wadau
walioyakusanya lengo kuwaongeza thamani katika sekta ya uvuvi.
Muumini
amesema ulaji wa Samaki kwa mtu mmoja mmoja ni Mdogo lakini kuna
kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu na walaji wanapendelea zaidi
migebuka kuliko aina nyingine za Samaki tofauti na kuhe pia bei ya
migebuka ni rahisi.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Dk
Ismael Kimerei amesema mtu akitumia mazao hayo kwa sasa hawezi kupata
virutubisho vya kutosha vilivyokisudiwa mwilini kutokana na kuandaliwa
chini ya kiwango.
Mapema Mkurugenzi wa Taasisi
hiyo ya TAFIRI, aliwaambia washiriki wa warsha hiyo kuwa wanalo jukumu
la kujadili na kuthibitisha utafiti uliofanywa kufuatilia mnyororo wa
thamani kwa uvuvi wa mazao ya samaki aina ya migebuka na dagaa katika
Ziwa Tanganyika.
Dk Kimerei alisema utafiti
huo umebainisha aina ya uvuvi unaofanyika Ziwa Tanganyika kuwa ni uvuvi
mdogo mdogo unoendeshwa na wavuvi wenye zana duni na kwamba uvuvi huo
bado haujahodhiwa na wavuvi wakubwa.
Alisema mradi
wa FISH4ACP unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka mitano na
kwamba mwaka wa kwanza (2020/2021) mradi umeshughulika na utafiti
kubainisha wadau wa sekta hiyo, shughuli zao, changamoto zinazowakabili,
maoni yao ili kuelewa aina ya uwekezaji, ramani walipo, mahala pa
kuanzia ili kuhkikish shughuli za uvuvi katika ziwa Tanganyika
zinakuja endelevu, “Tutakuja na mpango kazi wa miaka minne tukilenga
kujikita katika utekelezji wa mradi kikamilifu.” Dk Kimerei alifafanua.
Aidha
amesema waliweza kuwafikia watu 500 katika utafiti wao na kwamba
katika utafiti huo waliweza kubaini biashara ya mazao ya uvuvi inafanywa
na watu wa hali ya chini hivyo.
Amesema utafiti
huo utasaidia kuwapa matokeo chanya yatakayowasaidia kuwaboresha
mazingira rafiki kwa wafanyabiasha na wavuvi katika ziwa Tanganyika.
No comments:
Post a Comment