Na Mwandishi Wetu
NYOTA wa zamani wa Klabu ya Simba, Spier Mbwembwe pamoja na mashabiki wa klabu hiyo wameandaa michuano ya aina yake ndani ya Jimbo la Segerea kwa lengo la kuinua na kuendelea vipaji vya soka kwa vijana.
Michuano hiyo inavyokwenda kwa jina la 'Segerea Super Cup' imeanza kutimua vumbi juzi ndani ya Uwanja wa dogodogo ikijumlisha timu 16 ambazo zinashiriki michuano hiyo.
Mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo ulichezwa kati ya Songea FC na Segerea FC, ambao ndio wenyeji wa michuano hiyo. Timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo, mgeni rasmi Hope Kaiza, ambaye pia ni mdhamini wa mashindano hayo, alisema amevutiwa na mawazo ya wadau hao wa soka, ataunga mkono kuhakikisha Segerea inakuwa na vipaji vya kutosha.
Alisema kwa sasa mpira ni ajira kubwa kwa vijana hivyo wanatakiwa kuwekezewa ili kutumiza ndoto zao.
"Niko kwa hapa kwa sababu nina mapenzi na mpira hivyo nitakuwa nawasapoti vijana kwa kile nilichonacho, hii itasaidia vijana wa Segerea lakini pia Tanzania kwa ujumla kwa kuwa kijana yoyote atakayepata mafanikio ni kwa ajili ya Taifa zima.
"Jambo la msingi wazingatie malengo Kama wazazi na wadau tumeamua kujitoka kwa ajili yao nao wapambane ili kufikia ndoto zao," alisema Kaiza.
Aidha Kaiza alisema katika michuano hiyo kutakuwa na zawadi mbalimbali, ambapo mshindi wa kwanza atachukua mbuzi na wa pili jezi, pia kutakuwa na zawadi kwa mashabiki bora.
Mjumbe wa Kamati yaa maandalizi ya michuano hiyo Shebi Machumani, alisema uzalishaji wa wachezaji wakubwa sio jukumu la Shirikisho la Soka peke yake bali wadau ndio wanatakiwa kutia nguvu katika maeneo yao ili kuibua vipaji.
"Nashukuru Mungu kwanza maandalizi yalikuwa mazuri na wachezaji wote ambao wapo hapa wanaujua mpira naimani msimu ujao baadhi yao wataweza pata nafasi katika klabu mbalimbali," alisema Machumani. Alisema Machumani.
No comments:
Post a Comment