Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
WAZIRI wa Afya Mendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto DKt Doroth Gwajima amesema kuwa matumizi ya takwimu zenye ubora katika ngazi za chini zitasaidia kuweza kufanya maamuzi ya kisayansi kwani bado kuna changamoto katika halmashauri nchini kutokuwa na takwimu sahihi jambo ambalo linarudisha nyuma Sekta ya Afya.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dodoma katika madhimisho ya siku ya Epidemiolojia ya wataalamu wa Maabara nchini ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza Tanzania ambapo waziri huyo amesema kuwa ili kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na matukio yanayoathiri afya ili kutambua mapema viashiria hatari kwa jamii lazma pawepo na takwimu zenye ubora katika ngazi ya halmahauri.
Aidha waziri Gwajima ameeleza kuwa jumla ya watumishi mia tano kumi na mbili kutoka idara ya afya ya binadamu na idara ya afya ya mifugo wamepatiwa mafunzo katika ngazi ya kozi ya awali kutoka mikoa yote 26 na halmashauri mia moja hamsini na tisa kwa kipindi cha miaka sita.
Dkt.Gwajima amesema ni vyema kufanyika tathmini juu ya kazi wanazofanya wataalam zinaendana na makusudio ya mwongozo wa ajira na si kuwapangia kazi zingine.
Aidha,Dkt.Gwajima amesema matumizi ya takwimu bado ni changamoto katika sekta mbalimbali hapa nchini hivyo ni lazima watumishi kuzifanyia kazi takwimu na kufanya tafiti za kutosha.
Mkurugenzi wa kinga kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii ,jinsia,Wazee na watoto Dkt.Leonard Subi amesema zaidi ya watanzania 512 wamepatiwa mafunzo ya utaalam wa epidemiolojia na maabara katika mikoa yote 26 Tanzania bara .
kwa upande wake rais wa chama cha wataalamu wa epidemiolojia na maabara Tanzania (TANFLEA)dokta Elibariki Mwakapeje amesema kuwa wao kama TANFLEA ni kuhakikisha afya ya mtanzania inaimarika ili watu waweze kuwa na afya bora na Waendelee kufanya shughuli zao za kila siku.
Madhimisho haya ya siku ya Epidemiolojia ya wataalamu wa maabara yamefanyia kwa mara ya kwanza nchini Tanzania huku madhimisho hayo yakibewa na kauli mbiu isemayo kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na matukio yanayoathiri afya ili kutambua viashiria hatari kwa jamii.
No comments:
Post a Comment