Katibu
Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, akizungumza na wadau wa tasnia ya filamu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, amewataka wasanii nchini kushiriki kuiendesha tasnia kwa weledi, kujenga umoja na kuiongezea thamani wao wenyewe kwakutoa maoni ya kuboresha kila eneo badala ya kuwa walalamikaji miaka nenda rudi.
Dkt.
Abbasi amesema hayo leo Novemba 28, 2021, jijini Dar es Salaam wakati
alipokutana na kufanya mazungumzo na wadau wa tasnia ya filamu nchini
katika hatua za kujipanga zaidi kuelekea Tamasha la Tuzo za Filamu za
mwaka 2021 ambazo Serikali kupitia Bodi ya Filamu imeamua kuzirejesha na
zitafanyika mwaka huu kwa mara ya kwanza wakati pia tuzo za muziki na
sanaa nyingine nazo zikiwa jikoni.
Amewasisitiza
wasanii kuthamini tuzo hizo kwa kuwa zinalenga kuwatangaza ndani na nje
ya nchi pamoja na kuwapa hamasa ya kufanya kazi bora zaidi.
“Penye
kasoro tuambieni tutaboresha, ukikosa tuzo usinune angalia ulipojikwaa
mwakani ufanye vyema zaidi lakini kwa ujumla tuzo hizi ni za nchi wala
sio za mtu kwa hiyo tutasimamia haki na weledi,” alisema Dkt. Abbasi
kauli ambazo zimeungwa mkono nawadau hao wengi.
No comments:
Post a Comment